Header ads

Header ads
CLUB MASAI KAHAMA
» »Unlabelled » AFARIKI DUNIA KWA KUGONGWA NA ROLI KAHAMA

MTU mmoja Mkazi wa Kahama Mkoa wa Shinyanga Mwenyeasili ya Kihindi Ismail Mohamed Walu amefariki Dunia kwa kugongwa na Roli aina ya Fuso linalosomba mchanga lenye namba za usajili  T161 AQR mali ya Ndeleye Mkazi wa Kigoma.
Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Shinyanga Kihenya kihenya alithibitisha kupokea kwa taarifa hizo na kuongeza Tukio hilo lilitokea juzi majira ya saa tisa mchana wakati Mohamed akiwa anaendesha baiskeli akitokea bijampola kueleke Kahama mjini ndipo Gari hilo lilimgonga na kupoteza maisha hapohapo likiwa liaelekea Shunu.
Kamanda Kihenya alisema kuwa Chanzo cha ajali ni Mwendokasi aliokuwanao Dereva wa Roli hilo na alipomgonga marehemu huyo alilitelekeza Gari hilo na kwenda kusikojulikana na jeshi la Polisi mkoani humo linaendelea na jitihada za kumsaka Dereva huyo.
Hata hivyo Wananchi waliokuwa kwenye tukio hilo walisema Jeshi la usalama Barabarani Wilayani  humo limeshindwa kuyaondoa maroli Makubwa ambayo yanaegeshwa pembezoni mwa Barabara hizo ambapo yamekuwa yakisababisha ajali mara kwa mara kutokana na kuibana njia.
Maroli Makubwa ambayo yanaegeshwa pembezoni mwa Barabara

About Unknown

Kwa jina Naitwa MWEUSI waweza wasiliana nami namba 0757420837, 0629208856 au email: timotheosodoka@gmail.com
«
Next
Chapisho Jipya
»
Previous
Taarifa za zamani

Hakuna maoni:

Leave a Reply