Merina amelazwa Moi baada ya kupewa rufaa na Hospitali ya
Mwananyamala alipokuwa amelazwa awali, kutokana na majeraha hayo ambayo
yanadaiwa kusababishwa kung’atwa kwa meno na kupigwa kwa vitu
mbalimbali mara kwa mara.
Akizungumza kwa shida Merina alisema amekuwa katika hali ya mateso
tangu mwaka 2012, kwani bosi wake huyo ambaye anamtaja kuwa ni
mwanasheria mkazi wa Boko amekuwa na tabia ya kumpiga na vitu mbalimbali
akiwa amemvua nguo.
“Haya marejaha niliyonayo sasa, alinipiga kwa fagio la chooni
akamalizia na jagi, kisha akapiga simu nyumbani kwetu huko Ishozi Kiziba
mkoani Kagera, akawaambia wazazi kwamba amenikung’uta kichwa kwa sababu
mimi ni mjeuri,” alieleza Merina na kuongeza:
“Mara kwa mara amekuwa na tabia ya kunivua nguo na kunipiga na
chochote anachojisikia, ananing’ata kisha ananipakaza chumvi kwenye
majeraha,” alisema Merina.
“Mara zote anazonipiga huniambia kwamba sijafanya kazi vizuri au
sijamaliza kuzifanya, lakini mwanaye ambaye ninamlea huwa analia sana
akimwambia usimpige dada, mwachie,” alisema Merina.
Alibainisha kwamba dada wa mtuhumiwa huyo anayemtaja kwa jina la
Josephine Rwechungura, baada ya kukerwa na vitendo hivyo vya kikatili
alivyotendewa ndiye alimpeleka hospitali.
Merina alisema kuwa hajawahi kupewa malipo yake na bosi huyo ambaye
walikubaliana mshahara wa Sh40,000 na Sh20,000 hutumwa kwa wazazi wake
na zilizobaki alikuwa anadai kwamba anamwekea.
Moi yajitolea kumsaidia
Ofisa Uhusiano wa Moi, Patrick Mvungi alisema wamempokea Merina juzi
saa 7.00 usiku, baada ya kuelezwa historia ya majeraha yake uongozi
umeguswa na kujitolea kugharimia matibabu yake.
“Madaktari wamesema kwamba anatakiwa kufanyiwa kipimo kikubwa cha CTS
can ambacho kitawezesha kujua majeraha aliyonayo yana ukubwa gani,
gharama zake ni Sh250,000 ambazo Moi itazitoa na kumpatia matibabu
bure,” alisema Mvungi.
Awali Katibu Afya wa Hospitali ya Mwananyamala, Edwin Bisakala
alisema Merina alipelekwa hospitalini hapo Juni 11 mwaka huu na msamaria
mwema, baada ya madaktari kumwona walibaini kwamba ana majeraha
makubwa kichwani
Hakuna maoni: