Header ads

Header ads
CLUB MASAI KAHAMA
» »Unlabelled » KIJANA AUAWA NA WANANCHI KWA TUHUMA ZA WIZI WA TV NA SOLAR WILAYANI KAHAMA, .


Mwili wa Marehemu ukiwa eneo la tukio baada ya kuuawa
Kijana mmoja anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 28-30 ambaye hajafahamika jina lake wala makazi ameuawa na wananchi wanaodaiwa kuwa na hasira kwa tuhuma za wizi katika mtaa wa Muhongolo wilayani Kahama mkoani Shinyanga.

Tukio hilo limetokea jana majira ya saa tatu asubuhi baada ya kudaiwa kuwa mtuhumiwa huyo alikutwa ndani kwenye nyumba ya jirani ambayo hata hivyo haijatajwa, ambapo alijifungia ndani kabla ya wananchi kuvunja mlango na kumtoa.

Imedaiwa kuwa Kijana huyo amewawa akituhumiwa kuhusika na wizi wa TV na Solar katika maeneo ya mtaa huo, na kwamba amekuwa akifanya uhalifu mara kwa mara lakini amekuwa akiendelea kuonekana mtaani hata baada ya kukamatwa na polisi. 

Jeshi la Polisi wilaya ya Kahama limethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba Mwili wa Marehemu umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya Wilaya ya Kahama, huku upelelezi ukiendelea.


About Unknown

Kwa jina Naitwa MWEUSI waweza wasiliana nami namba 0757420837, 0629208856 au email: timotheosodoka@gmail.com
«
Next
Chapisho Jipya
»
Previous
Taarifa za zamani

Hakuna maoni:

Leave a Reply