 |
Hapa ni katika ukumbi wa Kapaya mjini Kahama mkoani Shinyanga ambako leo kumefanyika mkutano mkubwa wa Fursa "Tufanikiwe pamoja"ulioandaliwa
na kampuni ya uchimbaji madini ya dhahabu ya African Barrick
inayomiliki migodi ya Buzwagi na Bulyankulu wilayani Kahama kwa
kushirikiana na Clouds Media Groups na kukutanisha makundi mbalimbali ya
wananchi wakiwemo wasanii,wajasiriamali,wakulima,wafugaji na vikundi
vya wadau wa maendeleo.Lengo kuu ni kuwaelimisha na kuwahamasisha wakazi
wa Kahama kuchangamkia fursa mbalimbali zilizopo Kahama ambazo zinaweza
kuwapatia kipato ama kunyanyua vipato vyao.Mgeni rasmi katika huo
mkutano huo alikuwa mkuu wa wilaya ya Iramba mkoani Singida ndugu
Yahaya Nawanda
|
Kulia ni Afisa Mahusiano mgodi wa Buzwagi bi Doroth Bakule kushoto kwake ni mwandishi wa habari gazeti la Habari leo bwana Raymond Mihayo
 |
Awali
mkurugenzi mtendaji wa Clouds Media Group bwana Ruge Mutahaba
akizungumza katika mkutano wa Fursa mjini Kahama leo ambapo alisema
Tanzania ina rasilimali nyingi na mji wa Kahama unazo fursa nyingi na
unaendelea kwa kasi hivyo vijana wanapaswa kuzichangamkia ili
kujiendeleza huku akiwataka kutokata tamaa,kujiamini na kuwa na mawazo
ya mafanikio siku zote. |
 |
Wakazi
wa Kahama wakimsikiliza kwa makini mkurugenzi mtendaji wa Clouds Media
Group bwana Ruge Mutahaba ambaye alisema chochote kinachoizunguka jamii
ni fursa kwa mtu mwenye nia ya kupenda maendeleo na kwamba hakuna haja
ya kutafuta kitu kipya katika eneo linalokuzunguka bali ni kuangalia
namna ya kuziboresha ili ziweze kuzalisha kipato.Mutahaba aliwataka
wananchi kutokata tamaa kwa kukosa mitaji kwani kila kitu kinawezekana
kwani hata Clouds Media Groups ilianza kwa mtaji mdogo wakiwa na vyumba
viwili pekee na sasa wamefanikiwa kutokana na kutokata tamaa na kuwaza
kufanikiwa siku zote.
 |
Mgeni
rasmi katika mkutano huo wa fursa mkuu wa wilaya ya Iramba mkoani
Singida ndugu Yahaya Nawanda akizungumza na wakazi wa Kahama,ambaye ana
mradi wa kuku wilayani kwake,aliwataka wananchi kutobweteka na kukaa
vijiweni.
Alisema"Hakuna
serikali ambayo itakuletea maendeleo vijiweni,unayesubiri ikuletee
pesa,utakaa hadi utachoka,tafuteni fursa katika maeneo yenu,undeni
vikundi vya kuwaletea kipato"
Mkuu
wa wilaya ya Iramba mkoani Singida ndugu Yahaya Nawanda akizungumza na
wakazi wa Kahama leo ambapo pamoja na mambo mengine aliwaasa wakazi wa
Kahama kwa wabunifu kwa kuangalia nini kipo katika maeneo ambacho
kinaweza kuwaingizia kipato
 |
Meneja
wa mgodi wa dhahabu wa Buzwagi (unaomilikiwa na African Barrick Gold
Mine) ndugu Philbert Rweyemamu akizunguzungumza katika mkutano huo
ambapo alisema ABG kwa kushirikiana na Clouds Media Groups wameungana
pamoja na kukusanya wakazi wa Kahama hususani vijana ili kuwaeleza
kuhusu fursa zinazowazunguka.Rweyemamu alisema fursa inaanza pale mtu
anapotambua kuwa kuna fursa hivyo wakazi wa Kahama waangalie katika
mazingira yao nini kinahitajika ambacho kinaweza kuwaingizia kipato |
 |
Mkutano unaendelea |
 |
Meneja
wa mgodi wa dhahabu wa Buzwagi Philbert Rweyemamu alisema nchi jirani
za Uganda na Kenya zinazidi kuendelea kutokana na kwamba wao
wanachangamkia fursa hivyo kuwataka watanzania kuthubutu kuleta
mapinduzi badala ya kuendelea kulalamika kwamba ni maskini wakati
watanzania wanazo akili za kuweza kufanya mambo makubwa.Pia alitumia
fursa hiyo kuwakaribisha wakazi wa Kahama kufanya kazi na African
Barrick Gold Mine |
 |
Mbele
kulia ni afisa mahusiano mgodi wa dhahabu wa Buzwagi bi Blandina
Mughezi akifuatilia kilichokuwa kinajiri katika mkutano wa fursa "Tufanikiwe pamoja" |
 |
Wakala
wa mabasi katika stendi ya Kahama bwana Abdi Mohamed ambaye ni miongoni
mwa wakazi wa Kahama akichangia mawili matatu katika mkutano huo wa
fursa ambao umetumika kuwaamsha wakazi wa mji wa Kahama kuchangamkia
fursa zilizopo katika mazingira yao
 |
Mkutano wa fursa uliondaliwa na
kampuni ya uchimbaji madini ya dhahabu ya African Barrick kwa
kushirikiana na Clouds Media Groups umekutanisha mamia ya wakazi wa
Kahama
Pichani
aliyesimama ni mfanyabiashara na mkulima kutoka Kahama akiuliza swali
wakati wa mkutano huo wa Fursa mjini Kahama mkoani Shinyanga
Afisa
Mahusiano mgodi wa Buzwagi bi Doroth Bakule akizungumza katika mkutano
huo ambapo aliwataka wakazi wa Kahama kujiamini huku akiwakaribisha
kufanya kazi na African Barrick
 |
Mkutano
wa fursa unaendelea ambapo wakazi wa Kahama wameelimishwa na
kuhamasishwa kuchangamkia fursa mbalimbali zilizopo Kahama ambazo
zinaweza kuwapatia kipato ama kunyanyua vipato vyao na kuondokana na
umaskini katika jamii. |
 |
Mjasiriamali anayejishughulisha na usindikaji wa alizeti akizungumza katika mkutano wa fursa leo mjini Kahama |
 |
Kushoto
ni mkurugenzi mtendaji wa Clouds Media Group bwana Ruge Mutahaba akiwa
na msanii wa Movie Bad Boy,ambaye anajishughulisha na
uandishi,uigizaji,uongozaji na uzalishaji wa movie mbalimbali |
 |
Msanii
wa muziki Mwasiti Almas ambaye yuko kwenye fani ya muziki kwa miaka 8
sasa akizungumza katika mkutano huo ambapo aliwataka vijana wanaoingia
katika fani ya muziki kujituma,kuwa wavumilivu na kuwa na nidhamu
katika kazi hiyo kwani ni kama kazi zingine za ofisini |
 |
Msanii
Mwasiti akiwasisitiza wakazi wa Kahama hususani wanaopenda kazi ya
usanii kujitokeza na kuamini kuwa wanaweza lakini waingie kwa kutambua
kile wanachokifanya |
Msanii wa bongo fleva Joslin Abraham kutoka Kahama akichana mistari leo katika mkutano wa fursa ulioandaliwa na Clouds Media Groups na African Barrick Gold Mine
Kushoto ni mkurugenzi
mtendaji wa Clouds Media Group Ruge Mutahaba,kulia kwake ni msanii wa
bongo fleva Joslin Abraham kutoka Kahama ambaye alichana mistari katika
mkutano huo.Kijana huyo alionesha uwezo wake mkubwa katika muziki
pamoja na kwamba bado hajatoka.Mutahaba alitumia fursa hiyo kumtaka
msanii huyo kujitofautisha na wasanii wengine ili kufikia malengo yake
 |
Pichani
ni bi Seven Mosha msimamizi wa vipaji Afrika( PAN-AFRICA) ambapo
alisema ukitaka kuingia katika kitengo flani unapaswa kuelewa mambo
mengi kuhusu kitengo hicho hali ambayo itakuwezesha kutengeneza pesa
vizuri |
 |
Seven
Mosha aliwaasa wakazi wa Kahama kuamini kuwa kila kitu kinawezekana
endapo mtu ataweka jitihada za maksudi kufanikisha kile anachokifanyia
kazi

Katika
mkutano huo wa fursa wakazi wa Kahama waliohudhuria walikaa katika
vikundi mbalimbali kisha kujadili namna ya kutumia fursa zilizopo Kahama
ili kujiinua kiuchumi
|
Hakuna maoni: