Header ads

Header ads
CLUB MASAI KAHAMA
» »Unlabelled » MWANAFUNZI WA CHUO KIKUU ALIYECHOMWA MOTO AKIDHANIWA NI MWIZI AFARIKI DUNIA

Daniel Anael Lema, aliyekuwa mwanafunzi wa mwaka wa nne wa shahada ya sheria katika Chuo Kikuu Kishiriki cha Mt. Augustino, Tawi la Iringa (Ruaha University College – RUCO), amefariki dunia baada ya kushambuliwa kisha kuchomwa moto na wananchi wenye hasira akidhaniwa kuwa mwizi.
 
Tukio hilo lilitokea Juni 24, 2014, majira ya saa 5 usiku ambapo inadaiwa kuwa Daniel alikuwa ametoka kuangalia michuano ya Kombe la Dunia, akawa anatafuta chakula cha jioni ambapo alipofika kwenye mgahawa mmoja ambao ulikuwa umefungwa, aliingia ndani ambapo binti aliyekuwa amelala ndani ya mgahawa huo, alianza kupiga kelele za mwizi zilizowakusanya wananchi wenye hasira kali.
 
Wananchi hao walianza kumshambulia Daniel wakiongozwa na mlinzi mmoja wa jamii ya Kimasai, baada ya kuzidiwa na kichapo wananchi hao walimmwagia mafuta ya taa na kumchoma moto kisha wote wakatoweka.
 
Mwanafunzi huyo aliokolewa na madereva bodaboda ambao walizima moto na kumkimbiza katika Hospitali ya Rufaa ya Iringa lakini siku kadhaa baadaye alifariki dunia.
 
Mwili wa marehemu umeagwa mapema leo katika hospitali hiyo tayari kwa safari ya kuelekea mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya mazishi yatakayofanyika kesho Jumatano.
Jeneza lenye mwili wa marehemu Daniel Lema kabla ya kuagwa.
Jeneza lenye mwili wa marehemu Daniel Lema kabla ya kuagwa.
Daniel Anael Lema, aliyekuwa mwanafunzi wa mwaka wa nne wa shahada ya sheria katika Chuo Kikuu Kishiriki cha Mt. Augustino, Tawi la Iringa (Ruaha University College – RUCO) enzi za uhai wake

About Unknown

Kwa jina Naitwa MWEUSI waweza wasiliana nami namba 0757420837, 0629208856 au email: timotheosodoka@gmail.com
«
Next
Chapisho Jipya
»
Previous
Taarifa za zamani

Hakuna maoni:

Leave a Reply