Bw. Oka Constantine (35) akiwa amejeruhiwa na sururu.
Mwezi uliopita hapa Kandili Yetu tuliitoa habari hii mara mbili:
Ila
kutokana na uzito wa suala hili, bado kuna mambo mengi ya nyuma ya
pazia. Na leo hii tumeona itakua vyema tukishare nawe mdau wetu...Kwa
hisani ya GPL, Fuatilia updates hizo hapa chini..
TUKIO LA KUTISHA!
Habari
hiyo ilimhusu mwanaume mmoja ambaye jina halikupatikana kuwa alipigwa
shoka (baadaye ilibainika ni sururu) hadi kuzama kichwani upande wa
kushoto kwa madai ya kufumaniwa na mke wa mtu katika eneo ambalo pia
halikujulikana.
Kingine
katika habari hiyo, haikujulikana mara moja mtu huyo alikumbwa na tukio
hilo sehemu gani ya Tanzania lakini ilijidhihirisha kuwa ni hapa nchini
kutokana na shuka alilofunikwa akiwa hospitali kuandikwa; MSD. MSD
(Medical Stores Department) ni mashuka yanayotolewa na Serikali ya
Tanzania kwenye hospitali zake.
Picha ya X-ray ikionyesha surulu ilivyomjeruhi.
KILICHOBAINIKA
Siku
chache baada ya habari hiyo kutoka gazetini imebainika kwamba, mwanaume
huyo anaitwa Oka Constantine mwenye umri wa miaka 35, Risasi Jumamosi
lina ‘full story’.
KUMBE NI BUGANDO
Habari za uhakika zinasema kuwa, Oka amelazwa katika Hospitali Teule ya Bugando Mwanza.
Akizungumza
na gazeti hili juzi, mkurugenzi wa utawala na utumishi wa hospitali
hiyo, Leah Kagine alisema hali ya Oka bado haijatengemaa kwani bado hana
ufahamu wa kutambua wala uwezo wa kuzungumza.
“Huyo
mtu aliyepigwa shoka yupo hapa Bugando, hali yake bado. Hana ufahamu,
hawezi kuzungumza, labda urudi baada ya wiki mbili hivi unaweza kumkuta
amepata fahamu,” alisema Kagine.
Madaktari wakifanya upasuaji kuokoa maisha ya Bw. Oka Constantine.
UKUBWA WA JERAHA
Kagine
aliongeza kusema kuwa, kwa sasa bado ni vigumu kubaini ukubwa wa jeraha
hadi daktari atakapotathimini na kuthibitisha kulingana na maadili ya
kitabibu.
“Kuhusu
ukubwa wa jeraha ni vigumu kwa sasa kuzungumzia hilo, hadi hapo daktari
wake atakapofanya tathimini ya hali yake. Kisheria daktari ndiye
anayeweza kuzungumza mara baada ya tathimini kufanyika,” alisema
Kagine.
WALICHOKIFANYA MADAKTARI
Kwa
mujibu wa mmoja wa madaktari wa kitengo cha dharura hospitalini hapo,
Oka alifanyiwa upasuaji eneo la ubongo na kulazwa katika chumba cha
wagonjwa mahututi wanaohitaji uangalizi maalum (ICU).
Sururu iliyotolewa kutoka kwenye kichwa cha majeruhi.
MADAI YA KUPIGWA SHOKA
Kwa
mujibu wa watu waliodai kumfahamu Oka, anatuhumiwa kupigwa shoka katika
fumanizi na mke wa mtu na kupoteza fahamu hapohapo mpaka sasa.
ASILI YAKE
Uchunguzi
wa kina uliofanywa na gazeti hili umebaini kuwa, majeruhi huyo ni mkazi
wa Kijiji cha Miyombo, Kata ya Rwamgasa mkoani Geita.
KAZI YAKE
Ilizidi
kudaiwa kuwa, Oka ni fundi wa mashimo ya dhahabu alikuwa akifanya kazi
ya uchimbaji katika shimo Namba 41 ambalo kwa sasa limebadilishwa namba
hiyo na kuitwa Namba 1.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, ACP Joseph Konyo.
SIKU YA TUKIO
Siku
ya tukio, Oka alidaiwa kukutwa akiwa amekaa na mke wa mtu ndipo mwenye
mke akachukua sururu maarufu kwa jina la moko na kumpiga nayo kichwani
mpaka kuzama kisha akaondoka eneo la tukio kimyakimya, mkewe
alishakimbia.
Baada
ya kuanguka na kupoteza fahamu akiwa na damu chapachapa, wasamaria wema
walimpeleka kwenye Kituo Kidogo cha Polisi cha Rwamgasa na kisha
kukimbizwa Hospitali Teule ya Wilaya ya Sengerema (Sengerema DDH) ambako
alipewa matibabu ya dharura na kumhamishia Bugando.
MAKAMANDA WANAVYOPITWA NA MENGI
Awali na kwa nyakati tofauti makamanda wa
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Geita: “Nimepigiwa simu na waandishi wengi wakiulizia
tukio hilo. Niseme kwamba hapa mkoani kwangu halijaripotiwa. Kama lipo
ningewaambia, siwezi kuficha jambo kama hilo.” Anaitwa ACP Joseph
Konyo.
Kaimu
Kamanda Mkoa wa Mwanza, ACP Christopher Fuime: “Hakuna kitu kama hicho.
Unajua watu wa mitandao ya kijamii wanachukua vitu na kuweka kwenye
mitandao yao. Sijui hiyo wameitoa wapi?
Hakuna maoni: