Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Geita Joseph Msukuma
Na mwandishi maalum kutoka Geita
|
Siku
chache tu baada ya vyombo vya habari kuandika habari kuhusu mwenyekiti
wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Geita Joseph Msukuma kuhamasisha
wananchi kurudi na kuvamia eneo la mwekezaji Majaliwa
Maziku mwenye leseni lililoko katika kijiji cha Nyantorotoro wilayani
Geita mkoani humo,sasa mwenyekiti huyo ameibuka na kuanza kuwatishia
waandishi wa habari walioripoti habari hizo.
Akiongea
na waandishi wa habari kwa kuwapigia simu mmoja baada ya mwingine huku
akifoka amesema kuwa waandishi wote walioripoti habari hizo
atahakikisha anawaburuza mahakamani ili washike adabu kwani yeye
anawatetea wananchi wake.
Msukuma alisema kuwa waandishi hao wamekuwa wakitumiwa na mkuu wa ilawya ya Geita Omary Mangochie kwa kuandika mambo ambayo yanamchafua.
"Nyinyi
mnatumiwa na mkuu wa wilaya kwa kunichafua nitawaburuza mahakamani
nione kama huyo DC atakuja kuwatoa kwani ndiye anayewatuma
kuniandika",alisema Msukuma.
Hivi
karibuni Msukuma aliwahamasisha wananchi wasiokuwa na leseni kwenda
kuvamia eneo la mwekezaji na kuanza kufanya fujo kwa wafanyakazi wa
muwekezaji huyo ambapo walitimkia kusik julikana na jeshi la polisi
Wilaya ya Geita likingilia kati sakata hilo.
Hakuna maoni: