Mkurugenzi
wa Rino International Agency ambao ni Waratibu wa mashindano ya Urembo
ya Miss Tanzania,Hashim Lundenga akiongea na waandishi wa
habari juu ya sakata la umri halali wa Mrembo aliyetwaa taji hilo Mwaka huu, Sitti Mtemvu (kushoto).
Kamati
ya Miss Tanzani imesema kuwa haiwezi kumvua taji Miss Tanzania 2014
Sitti Mtemvu kwa kuwa ni Miss halali na mwenye vigezo vyote
vilivyotakiwa.
Akifafanua
kuhusu suala la umri, mratibu wa mashindano hayo Hashim Lundenga
amesema kuwa cheti halali walichonacho wao ni kile kinachoonesha Sitti
Mtemvu kazaliwa 24 mei 1991 na si vinginevyo.
Kuhusu suala la passport na leseni zilizosambaa kwenye mitandao ya jamii
zikionesha amezaliwa mwaka 1989, Lundenga amesema wao huwa hawangaali
vitu hivyo wanachojali ni cheti cha kuzaliwa.
Kuhusu tuhuma za unene amesema wao huwa hawaangalii wembamba wala ufupi, muhimu ni awe na vigezo vinavyotakiwa.
Hakuna maoni: