INAUMA sana! Baadhi ya ndugu waliokuwa wakiuaga mwili wa Aron Kihundwa (28) kwenye Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dar walijikuta wakidondoka na kuzimia kufuatia uchungu wa kumpoteza mpendwa wao huyo aliyedaiwa kuuawa na Komandoo wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania, Octavian Mgowele.
Tukio hilo lilijiri wiki iliyopita na kumfanya Mchungaji Elaina Msuya
wa Kanisa la KKKT aliyekuwa akiongoza misa ya kumuombea marehemu huyo,
kuingilia kati na kusema mwili usiendelee kuagwa ili kuzuia watu kuzidi
kuzimia.
Komandoo Octavian Mgowele mwenye cheo cha Luteni wa Kikosi cha 94 KJ
Ngerengere, Morogoro, Oktoba 13, mwaka huu alidaiwa kumuua Aron kwa
kumpiga kipigo kibaya.
Tukio hilo lilidaiwa kutokea kwenye baa iitwayo
Mbondela iliyopo Yombo - Buza maeneo ya Kipera, jijini Dar kwa madai
kwamba alikuwa akimbughudhi mke wa komandoo huyo.
Taarifa toka kwa mtu aliyekuwepo kwenye baa hiyo zinasema siku hiyo
mjeshi huyo alikaa meza moja na mkewe ambaye alitoka kufunga naye ndoa
jana yake.
Pia kwenye meza hiyo alikaa Aron huku wakiendelea kunywa bia
ambapo mnunuaji mkuu alikuwa komandoo.
Ikadaiwa kuwa, kuna wakati komandoo alikwenda kaunta aliporudi
alishangaa kumkuta mkewe amehama katika kiti alichomuacha.
Chanzo hicho
kikaendelea kusema komandoo huyo alimuuliza mkewe kisa cha kuhama kiti,
naye akamjibu; si huyu rafiki yako ananisumbua.’
Pi kuna taarifa zinasema kuwa kijana huyo alidaiwa kumshika kiuno shemeji yake ndiyo maana akahama kwenye kiti.
Wakati huo, marehemu alikuwa anauchapa usingizi kutokana na kulewa.
“Marehemu akiwa usingizini alishtukia komandoo akimwadhibu bila kujua sababu ni nini hadi akamjeruhi.
”Baada ya kumpiga sana hadi kumjeruhi tulimchukua marehemu na kumpeleka
Kituo cha Polisi Chang’ombe (Dar) na kupewa PF3, tukamkimbiza Hospitali
ya Temeke, ilipofika saa kumi usiku wa kuamkia kesho yake alifariki
dunia.
“Aron ni rafiki yake sana komandoo, hata siku ya ndoa yake, yeye ndiye
aliyempambia gari la harusi na ukumbi.
Siku ya tukio ilikuwa ni sherehe
ya kuvunja kamati.
“Hatujajua ni kwa nini komandoo aliamua kumpiga Aron kiasi kile, mambo
ya kuambiwa na mwanamke siyo ya kuyafanyia kazi kama haukushuhudia ama
hauna uthibitisho,” alisema shuhuda huyo.
Marehemu Aron alizikwa Oktoba 18, mwaka huu kijijini kwao Kyengia Wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro.
Hakuna maoni: