Wanawake wengi walikerwa na kitendo hicho wakisema kuwa kila mwanamke ana haki ya kuvalia mavazi yanayomfurahisha.
Hiyo
wiki jana kanda ya video ilisambazwa kwa mitandao ya kijamii ikionyesha
mwanamke huyo ambaye hakutajwa jina hadi sasa akivuliwa nguo zake na
wanaume katika kituo cha magari ya abiria kati kati mwa Nairobi.
Wanawake
mashuhuri wakiwemo wasanii, wanasiasa na wanaharakati walilaani kitendo
hicho wakihoji kwani mavazi ya mwanamke yanamhusu nini mwanamume ambaye
sio mumewe wala jamaa yake.
Baadhi walikitaja kitendo hicho kuwa cha kinyama na kinachokiuka haki za wanawake.
Msanii
mmoja mashuhuri Nyota Ndogo alinukuliwa akisema ikiwa wanaume wanawavua
nguo wanawake kwa kile wanachosema ni mavazi yasiyo ya kiheshima, basi
na wanaume wanaolegeza long'i zao na wao basi pia wavuliwe nguzo zao.
Hakuna maoni: