Na Joseph Ngilisho, Arusha
MREMBO Mariam
Mohamed ambaye alishiriki na kushika nafasi ya pili ya Shindano la Miss
Mara mwaka 2003, wiki iliyopita alizusha vurumai kubwa kwa kuzichapa
kavukavu na mumewe usiku baada ya kumkuta akiwa na baamed ndani ya
nyumba moja iliyopo Njiro eneo linalojulikana kama Nguzo Moja jijini
Arusha, Amani lina mkanda kamili.
Licha
ya kuzichapa na mumewe huyo ambaye ni mfanyabiashara aitwaye Rasha
Idrisa (38), mkazi wa Sinza jijini Dar es Salaam, baamed huyo aitwaye
Prisila, naye alipata kipigo kikali toka kwa Miss huyo aliyekuwa
akisaidiana kutoa dozi na mpambe wake.
Prissila
anayefanya kazi kwenye baa moja iliyopo maeneo ya Njiro (jina
linahifadhiwa) alijaribu kujitetea kuwa hakufahamu kama mpenziwe huyo
alikuwa mume wa mtu, alishambuliwa sehemu mbalimbali za mwili wake,
ikiwa ni pamoja na kukabwa shingo, hali iliyomuacha hoi na kuapa
kutoendelea tena kuiba vya watu.
Operesheni
Fichuo Maovu (OFM) ya Global Publishers ilitonywa mapema juu ya kuwepo
kwa mpango wa kumfumania Rasha, anayedaiwa kuwa alisafiri kibiashara
akimuaga mkewe kuelekea Zambia, tokea Agosti mwaka huu.
Chanzo
chetu kinadai kuwa kitu kilichompa mashaka Mariam ni wakati alipokuwa
akiwasiliana kwa simu na mumewe, kwani miito yake ilionyesha kuwa
mpigiwaji alikuwa nchini. Baada ya kuona hivyo akaanza udadisi wa kujua
ni wapi hasa alipo mumewe.
Siku
chache zilizopita, chanzo hicho kilisema msichana huyo alipata taarifa
kutoka kwa marafiki zake waliopo Arusha, juu ya kuonekana kwa mumewe
akila maisha na msichana mmoja mhudumu wa baa, na kwamba alikuwa
akitanua naye kila siku na mara nyingi walilala pamoja.
“Mariam amepanga kesho ndiyo aende akawafumanie, kama ni pale baa au wanakoendaga, kwa hiyo nyinyi mnaweza kwenda pale ili mjue kitakachoendelea,” chanzo chetu kiliwasiliana na OFM ambao walifika katika baa anayofanya kazi Prisila bila yeye kufahamu na baadaye Mariam akiwa na mpambe wake nao waliwasili.
Baamedi, Prisila akipokea kichapo kutoka kwa rafiki wa Mariam Mohamed kwa kula ujana na mume wa mtu.
“Mariam amepanga kesho ndiyo aende akawafumanie, kama ni pale baa au wanakoendaga, kwa hiyo nyinyi mnaweza kwenda pale ili mjue kitakachoendelea,” chanzo chetu kiliwasiliana na OFM ambao walifika katika baa anayofanya kazi Prisila bila yeye kufahamu na baadaye Mariam akiwa na mpambe wake nao waliwasili.
Akiwa
hatambui kama anafuatiliwa, Prisila pamoja na rafiki yake mmoja ambaye
hakufahamika jina lake, waliondoka eneo hilo na kwenda kupanda daladala
lililokuwa likielekea Njiro na kuteremka eneo la Nguzo moja. Mariam naye
aliondoka na kuchukua usafiri binafsi kwa ajili ya kuwafuatilia
wasichana hao huku nyuma yao wakiwa OFM.
Prisila
aliingia katika nyumba moja iliyokuwa na geti jeusi majira ya saa tatu
na muda mfupi baadaye Mariam na mpambe wake nao waliwasili na kuukuta
mlango ukiwa wazi.Baada ya kuingia ndani, waliwakuta wawili hao wakiwa
katika mkao wa kimahaba na mara moja Mariam akiwa na fimbo, alianza
kumchapa mumewe aliyejaribu kumsihi kwa kupiga magoti ili walimalize
jambo hilo kwa mazungumzo. Wakati mume akipigwa na mke, mpambe alikuwa
akimpa kichapo cha maana Prisila.
Rasha
hata hivyo, baadaye alifanikiwa kumnyang’anya fimbo mkewe huyo na
kuanza kutoa vitisho kwa OFM waliokuwa wakipiga picha za tukio hilo.
Akizungumza wakati wa sekeseke hilo, Mariam alisema amekuwa akimfumania
mumewe mara kwa mara akiwa na wanawake tofauti na mara zote huomba
msamaha.
Ingawa
hawajafunga ndoa, Mariam alisema alianza kuishi na mwanaume huyo tangu
mwaka 2004 na kwamba maisha yao yametawaliwa na migogoro kutokana na
ukware wa mumewe.
Kwa upande wake, Rasha alisema yupo tayari kuachana na mkewe ili awe huru na maisha yake.
Kwa upande wake, Rasha alisema yupo tayari kuachana na mkewe ili awe huru na maisha yake.
Hakuna maoni: