Header ads

Header ads
CLUB MASAI KAHAMA
» »Unlabelled » BODABODA ACHINJWA BAADA YA KUFUMANIWA HUKO MOROGORO

Wimbi la mauaji yanayohusishwa na matukio ya mafumanizi yanazidi kushika kasi mkoani Morogoro ambapo mwishoni mwa wiki iliyopita dereva mwingine wa bodaboda aliyetajwa kwa jina moja la Kambi (33), anadaiwa kuchinjwa na kufa papohapo huku kifo chake kikihusishwa na matukio hayo.
 
Marehemu Kambi enzi za uhai wake.
Tukio hilo lilitokea juzikati majira ya saa 11:00 alfajiri ambapo mwili wa bodaboda huyo uliokotwa maeneo ya Modeko jirani na Makutano ya Barabara za lringa na Mazimbu na kusababisha mkewe kuchanganyikiwa huku ndugu wakiwa hawaamini.
 
Mke wa marehemu akiwa mwenye huzuni kubwa.
Muda mfupi baada ya tukio hilo, mwanahabari wetu alifika eneo la tukio na kuushuhudia mwili wa jamaa huyo ukiwa umetupwa lakini hawakuchukua chochote kutoka kwa marehemu huku wakimwachia bodaboda yake na waleti ikiwa na fedha taslimu shilingi laki 240,000.
 
Ndugu wa marehemu Kambi.
Kufuatia hali hiyo baadhi ya watu walioshuhudia tukio hilo, walidai huenda jamaa huyo alifumaniwa na mke wa mtu kwani mara ya mwisho alionekana akiwa amempakiza mwanamke hivyo kuna madai kwamba mwenye mali hakuwa na sababu ya kuchukua chochote zaidi ya kumtoa roho.Majira ya saa 12:00 asubuhi, polisi walifika eneo hilo la tukio na kuuchukua mwili wa marehemu na kuupeleka mochwari kwenye Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro.
 
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, SACP Leonard Paul.
Baada ya tukio hilo, mwanahabari wetu kusaka undani wa kifo cha bodaboda huyo. Kwenye eneo la tukio, ilidaiwa kwamba jamaa huyo aliuawa katika tukio lililohusisha fumanizi la mke wa mtu kwani baada ishu hiyo wahusika walitoka nduki bila kuchukua Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, SACP Leonard Paul alithibitisha kutokea kwa mauaji hayo.

About Unknown

Kwa jina Naitwa MWEUSI waweza wasiliana nami namba 0757420837, 0629208856 au email: timotheosodoka@gmail.com
«
Next
Chapisho Jipya
»
Previous
Taarifa za zamani

Hakuna maoni:

Leave a Reply