| ||
Afisa habari mkoa wa Shinyanga Magdalena Nkulu |
Licha ya serikali kusisitiza mambo yanayofanywa na serikali
yatangazwe na vyombo vya habari,hali imekuwa tofauti mkoani Shinyanga kutokana
na afisa habari mkoani humo Magdalena Nkulu kuwa na tabia ya kubagua
waandishi wa habari na wakati mwingine yeye mwenyewe kuandika habari na kutuma
kwenye vyombo vya habari.
Wakizungumza leo kwa nyakati tofauti waandishi wa habari
mkoani humo walisema wanasikitishwa na kitendo cha afisa habari huyo ambaye
kimsingi anatakiwa kuwa na mahusiano mazuri na waandishi wa habari badala yake
yeye amekuwa akifanya kinyume kwa kubagua waandishi wa habari.
Walisema kutokana na tabia hiyo ya afisa habari huyo ya
Umimi ndiyo maana miradi mingi ya maendeleo mkoani Shinyanga haijulikani kwa
wananchi kitendo kinachosababisha wananchi wailalamikie serikali kutowajali
kumbe tatizo ni kutangazwa kwa miradi hiyo.
“Huyu afisa habari tumemchoka,haiwezekani kila siku
inapotokea kazi za serikali yeye anabagua waandishi wa habari,anaalika marafiki
zake tu na wakati mwingine anajiandika kwenye fomu za waandishi wa habari ili achukue posho na
baadaye anatuma habari kwa kila mwandishi wa habari,Je hii ndiyo kazi ya uafisa
habari”,alihoji mmoja wa waandishi hao.
“Hata waandishi wa habari wa vyombo vya habari vya serikali
ikiwemo gazeti la Uhuru,nao wanabaguliwa,Huyu afisa habari amekuwa akisema
Gazeti limepitwa na wakati,na kutotakiwa kwenye shughuli zote muhimu za
serikali kama vile Ukaguzi wa miradi,ziara za mkuu wa mkoa,mawaziri
wanapokuja,kamati za bunge japokuwa ndiyo lenye Ilani iliyoahidiwa na chama
tawala “,aliongeza Chibura Makorongo,mwandishi wa habari gazeti la Uhuru na
Mzalendo.
“Hata kikao cha juzi na jana cha Bodi ya Barabara na cha
Kamati ya Ushauri ya mkoa, afisa habari alialika waandishi wa habari wanne pekeee,wakati
vikao hivyo ni muhimu,huu ni ubaguzi wa hali ya juu kwani ukiangalia hata
ualikaje wake ni wa ajabu,anaalika kwa kutuma ujumbe mfupi wa maandishi ya
simu(SMS),huu siyo utaratibu kwanza alitakiwa aandike barua kwa uongozi wa
chama cha waandishi wa habari”,aliongeza mwandishi mwingine.
Waandishi hao wa habari walisema pamoja na kuhudhuria vikao
hivyo vya bodi ya barabara na kile cha kamati ya ushauri ya mkoa kilichoanza
saa 4 asubuhi hadi saa 2 usiku ,siku ya Jumanne,April 14,2015 waandishi wa
habari waliolipwa na waandishi wa habari Wanne pekee wakati waandishi wengi tu
walikuwepo kwenye kikao hicho.
“Wajumbe wa kikao wote walipewa posho,lakini waandishi wa
habari wakaambulia patupu,na wakati mwingine hata maji ya kunywa kwenye vikao
huwa wananyimwa”,waliongeza.
Waandishi hao wa habari walisema kuna kipindi panapotokea
ziara ya viongozi wa serikali kama vile mawaziri na mkuu mkoa wa mkoa waandishi wa habari hawapewa taarifa,na
ikitokea wakapata taarifa huambiwa watafute usafiri wao hivyo kuwepo ugumu wa
mambo mazuri kuandikwa.
Hata hivyo mwanzoni mwa mwaka huu 2015 mkuu wa mkoa Ally Rufunga aliitisha mkutano wa Waandishi wa Habari (Press
Conference) lakini waandishi wa habari
hawakwenda kutokana na sababu ya kukithiri kwa manyanyaso hayo na
kutothaminiwa.
Kutokana na hali hiyo hivi sasa waandishi wa habari mkoani Shinyanga wana mgomo baridi na kususia
kazi za mkoani kwa sababu ya mahusiano mabaya na ofisi ya mkoa.
Naye
katibu wa waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga kareny masasy
alipopelekewa malalamiko hayo na waandishi wa habari aliyapokea na
kusema kuwa atayafanyia kazi.
Hata hivyo mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Rufunga alipotafutwa kwa njia ya simu kutokana na kutokuwepo ofisini,kwa ajili ya malalamiko hayo,alisema yuko kwenye gari.
Habari tulizozipata pia katika halmashauri za wilaya mbalimbali baadhi ya maafisa habari wamekuwa miungu watu kwa kuwanyanyasa waandishi wa habari kwa kuendekeza ubaguzi.
Hakuna maoni: