MWANAMITINDO na
mtangazaji maarufu Bongo, Jokate Mwegelo amewagomea wagombea urais wote
waliotangaza nia cha kuingia ikulu Oktoba, mwaka huu.
Mwanamitindo na mtangazaji maarufu Bongo, Jokate Mwegelo.
Jokate aliyasema hayo
alipoulizwa na Global TV Online Ijumaa iliyopita kuhusu kuelekea
Uchaguzi Mkuu 2015 kuwa, amejiandaaje na yupo kambi gani kati ya
wagombea urais waliotangaza nia na wale ambao bado.“Hadi sasa sipo
katika chama chochote na sitaki kuitwa wala sitegemei kujiunga na timu
yoyote ya wagombea urais wa mwaka huu,” alisema Jokate.
Wagombea wanaotarajiwa
kuingia kwenye kinyang’anyiro cha urais ni Edward Lowassa (CCM), Benard
Membe (CCM), Mwigulu Mchemba (CCM), January Makamba (CCM), Dk. Slaa
(Chadema), Ibrahim Lipumba (Cuf) na wengine wengi.
Hakuna maoni: