Hapa
ni katika uwanja wa taifa Mjini Kahama mkoa wa Shinyanga ambapo Shirika
la Kitanzania lisilo la kiserikali la Ariel Glaser Pediatric Aids
Healthcare Initiative(AGPAHI) linalojihusisha na mapambano dhidi ya
Virusi vya UKIMWI na UKIMWI limefanya Bonanza la Michezo kwa
vijana.Bonanza hilo limewakutanisha vijana 120 kutoka Vituo vya Afya
vilivyopo katika halmashauri ya wilaya ya Ushetu,Msalala na Kahama Mji.
Bonanza
hilo lililofanyika Jumamosi,Mei 21,2016 liliandaliwa na AGPAHI
likiwezeshwa na Mfuko wa Kusaidia watoto wa Uingereza ( Children’s
Investment Fund Foundation UK- (CIFF) limekutanisha vijana wenye umri
kati ya miaka 15 hadi 19,ambao wapo katika rika balehe,rika ambalo ni
muhimu sana katika jamii.
Mgeni
rasmi katika Bonanza hilo la Michezo alikuwa Mkuu wa wilaya ya Kahama
Mheshimiwa Vita Kawawa.Wengine waliohudhuria Bonanza hilo ni waganga
wakuu wa halmashauri za wilaya ya KahamaMji,Ushetu na Msalala,wasimamizi
wa klabu za vijana,vijana,wafanyakazi wa AGPAHI na wakazi wa Kahama.
Awali
akisoma risala wakati wa Bonanza hilo,Mratibu Miradi kutoka AGPAHI, Dr.
Amos Scott alisema shirika lake linajitahidi kuwashirikisha vijana wa
rika balehe katika michezo na kuwapatia habari na elimu sahihi kuhusu
huduma rafiki za afya ya uzazi katika maeneo mbalimbali ambako shirika
linafanya shughuli zake.
“Bonanza
hili la michezo linahusisha vijana 120 wanaotoka kwenye klabu 9 za
vijana za Kituo cha afya
Ushetu,Bulungwa,Ukune,Lunguya,Chambo,Chela,zahanati ya
Kagongwa,Hospitali ya Mji wa Kahama na zahanati ya Segese zilizopo
katika halmashauri za wilaya ya Ushetu,Msalala na Kahama Mji ambazo
zinasimamiwa na AGPAHI kwa kushirikiana na halmashauri za wilaya
husika”,alieleza Dr. Scott.
Alisema lengo la bonanza hilo la michezo ni kutoa burudani kwa vijana,kuleta furaha,matumaini na kujenga urafiki baina yao.
“Vijana
hawa wanapokuwa katika klabu zao,tumekuwa tukiwapatia
vitabu,vipeperushi,mikanda ya video na kadhalika ili kuwapatia elimu
zaidi juu ya afya ya uzazi ,tunawasisitiza viongozi wa afya ngazi ya
halmashauri za wilaya kuhakikisha kuwa vijana wanaendelea kupata elimu
sahihi kuhusu afya ya uzazi ili waweze kufanya maamuzi sahihi”,aliongeza
Dr. Scott.
Akifungua
Bonanza hilo la Michezo, mkuu wa wilaya ya Kahama,Mheshimiwa Vita
Kawawa alilipongeza shirika hilo kwa kuwajali vijana kwa kuwakutanisha
ili wajifunze kupitia michezo.
“Natumia
fursa hii kwa namna ya pekee kabisa kulishukuru shirika la AGPAHI kwa
kuendelea kuwa karibu na hawa vijana,niwapongeze pia kuanzisha klabu za
vijana ambao mmekuwa mkiwakutanisha kila mwezi ili wajifunze kwa pamoja
masuala mbalimbali kama vile masuala ya rika kwa vijana na kushirikiana
katika kutatua changamoto zao za afya ya uzazi na Virusi vya UKIMWI na
UKIMWI”,alisema Kawawa.
Katika
hatua nyingine Mheshimiwa Kawawa alitoa wito kwa viongozi wa
halmashauri za wilaya husika kuendelea kutoa ushirikiano kwa shirika la
AGPAHI hususani katika kutekeleza majukumu ya kuwasaidia wananchi katika
huduma za afya hasa kwa watu wanaopata tiba na matunzo ili huduma
zipatikane katika ubora na ziwe rafiki kwa wananchi.
Miongoni
mwa michezo katika Bonanza hilo ni pamoja na mpira wa
miguu,riadha,kuvuta kamba,kukimbia na mayai,kukimbiza kuku,kucheza
muziki,kunywa soda kwa haraka zaidi,mbio za magunia na kuimba ambapo
kila mshindi na washiriki wote walipatiwa zawadi hali iliyoongeza furaha
zaidi kwa vijana hao.
Mwandishi
wetu Kadama Malunde alikuwepo katika Bonanza hilo la Michezo kuanzia
mwanzo hadi mwisho,ametuletea matukio katika picha. Fuatilia hapa….
Kabla ya Michezo Kuanza-Mratibu
Miradi kutoka AGPAHI Dr. Amos Scott akisoma risala kwa mgeni rasmi
(mkuu wa wilaya ya Kahama Mheshimiwa Vita Kawawa) katika Bonanza la
Michezo lililokutanisha vijana 120 kutoka vituo vya afya,zahanati na
hospitali katika halmashauri za wilaya za Ushetu,Msalala na Kahama Mji
mkoani Shinyanga
Vijana
kutoka katika Halmashauri ya wilaya ya Ushetu,Kahama Mji na Ushetu
wakiwa uwanjani kwa ajili ya Bonanza la Michezo lililoandaliwa na
shirika la AGPAHI
Aliyesimama
ni Mratibu Miradi kutoka AGPAHI Dr. Amos Scott akisoma risala kwa mgeni
rasmi,ambaye ni mkuu wa wilaya ya Kahama Mheshimiwa Vita
Kawawa(kulia),kushoto ni Afisa Miradi Kutoka AGPAHI Sipemba Julius.Dr
Scott alisema Bonanza hilo linatoa fursa kwa vijana kufurahi,kujifunza
kushirikiana,kufahamiana na kupata marafiki
Aliyesimama
ni Kaimu Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Mji Kahama Dr.George Masasi
akimkaribisha mgeni rasmi Mheshimiwa Vita Kawawa (Kushoto),kulia ni
Mganga mkuu wa halmashauri ya wilaya ya Msalala Dr. Hamidi Nyembea
Aliyesimama
ni Mkuu wa wilaya ya Kahama Mheshimiwa Vita Kawawa akifungua Bonanza la
Michezo katika uwanja wa taifa mjini Kahama ambapo alilishukuru Shirika
la AGPAHI kwa kuandaa Bonanza hilo huku akiliomba shirika hilo kuona
umuhimu wa kuwasaidia vijana wenye vipaji katika michezo
Mkuu
wa wilaya ya Kahama Mheshimiwa Vita Kawawa akizungumza wakati wa
kufungua Bonanza la Michezo ambapo aliwataka vijana kuonesha vipaji vyao
pia kujifunza kupitia michezo
Mkuu
wa wilaya ya Kahama Mheshimiwa Vita Kawawa akiteta jambo na Kaimu
Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Mji Kahama Dr.George Masasi (katikati)na
Mganga mkuu wa halmashauri ya wilaya ya Msalala Dr. Hamidi Nyembea
(kulia)
Bonanza ndiyo linaanza-Mkuu
wa wilaya ya Kahama Mheshimiwa Vita Kawawa akionesha kipaji chake cha
kucheza na mpira wakati wa kukagua timu za mpira wa miguu za klabu za
vijana kutoka halmashauri ya Mji Kahama,Ushetu na Msalala
Mkuu
wa wilaya ya Kahama Mheshimiwa Vita Kawawa akishikana mkono na
wachezaji wa Timu ya Vijana kutoka Halmashauri ya Mji wa Kahama wakati
wa kukagua timu hiyo
Mkuu
wa wilaya ya Kahama Mheshimiwa Vita Kawawa akishikana mkono na
wachezaji wa timu ya mpira wa miguu ya vijana kutoka halmashauri ya
Msalala
Wachezaji
wa timu ya vijana kutoka halmashauri ya Ushetu wakifanya mazoezi kabla
ya kuungana na vijana wa timu ya vijana kutoka halmashauri ya wilaya ya
Msalala kuikabili timu ya vijana wa halmashauri ya wilaya ya Kahama Mji
Mkuu
wa wilaya ya Kahama Vita Kawawa akiwaasa vijana kucheza mchezo wa
amani.Mchezo huo wa mpira wa miguu ulikuwa kati ya Timu ya Vijana kutoka
Halmashauri ya Ushetu walioungana na Vijana wa timu ya vijana kutoka
halmashauri ya wilaya ya Msalala dhidi ya timu ya vijana wa halmashauri
ya wilaya ya Kahama Mji.
Mkuu
wa wilaya ya Kahama Mheshimiwa Vita Kawawa akifungua Mchezo wa Mpira wa
Miguu kwa penati aliyoielekeza kwa golikipa wa timu ya vijana kutoka
Ushetu
Hata hivyo shuti kali la Mkuu wa wilaya ya Kahama Mheshimiwa Vita Kawawa liliishia kwenye mwamba
Kabla ya mchezo kuanza Mgeni rasmi Mheshimiwa Vita Kawawa na wafanyakazi wa AGPAHI wakapiga picha ya kumbukumbu
Mgeni
rasmi Mheshimiwa Vita Kawawa akiwa katika picha ya pamoja na
wafanyakazi kutoka halmashauri za wilaya ya Kahama Mji,Ushetu na Msalala
pamoja na wafanyakazi wa AGPAHI na wachezaji timu ya vijana wa
halmashauri ya Mji wa Kahama
Mgeni
rasmi Mheshimiwa Vita Kawawa akiwa katika picha ya pamoja na
wafanyakazi kutoka halmashauri za wilaya ya Kahama Mji,Ushetu na Msalala
pamoja na wafanyakazi wa AGPAHI na wachezai timu ya vijana wa
halmashauri ya Mji Msalala
Mchezo
katia ya Msalala na Ushetu Vs Kahama Mji ukaendelea ambapo kipindi cha
kwanza walicheza dakika 15 na kipindi cha pili dakika 15 na mpaka dakika
30 za mchezo zinamalizika Kahama Mji walijipatia magoli Matano huku
Msalala na Ushetu wakiambulia pamoja na kwamba waliungana pamoja
Mchezo
wa kukimbia na mayai nao ukachukua nafasi yake...ambapo Helena kutoka
Kahama Mji (kushoto) aliibuka mshindi na kupata zawadi ya begi la shule
Shindano
la Kuvuta kamba likaendelea...kati ya vijana kutoka Kahama Mji dhidi ya
vijana wa Ushetu na Msalala,ambapo walitoka droo baada ya kamba
kukatika
Mchezo
wa kukimbia kwenye magunia nao ulikuwepo..Vijana wa Kiume kutoka
Ushetu,Msalala na Kahama mji wanaonesha vipaji vyao.Katika mchezo huo
Peter Kulwa kutoka Kahama Mji aliibuka mshindi na kupewa zawadi ya begi
la shule
Vijana
wa kike nao hawakuwa nyuma katika mchezo wa kukimbia kwenye
magunia,ambapo Suzy John (katikati) kutoka Msalala aliibuka mshindi na
kupewa zawadi ya begi la shule
Shindano la kufukuza kuku...ukimkamata anakuwa wako...
Kijana Faustine Daudi kutoka Msalala akiwa ameshikilia kuku wake baada ya kuwashinda wenzake
Kwa upande wa vijana wa kike Jesca Robert kutoka Kahama Mji akakamata kuku..alisikika akisema "Kesho nakula supu ya kuku huyu"
Shindano
la Riadha/mbio za mita 100,pichani ni washindi kundi la wanaume..Wa
kwanza ni Ibrahim Bure kutoka Kahama Mji,wa pili Oscar Onesmo kutoka
Kahama Mji na wa tatu ni Faustine Daudi kutoka Msalala.Mshindi wa kwanza
alipata zawadi ya saa ya mkononi.Kwa upande wa kundi la wasichana
aliyeibuka mshindi ni Neema Bundala kutoka Msalala ambaye pia alipata
zawadi ya saa ya mkononi
Shindano la kunywa soda kwa haraka kwa vijana wa kiume.Mshindi alikuwa Patrick Marco (kushoto) kutoka Msalala
Shindano la kunywa soda kwa haraka kwa vijana wa kike..Mshindi alikuwa Suzy John (katikati) kutoka Msalala
Shindano la kucheza muziki-Vijana wote wakaingia uwanjani kucheza muziki
Tunaangalia jinsi vijana wanavyocheza muziki...
Vijana wakicheza wimbo wa Alikiba "Nasema Nao"
Vijana wakiendelea kucheza muziki
Muda wa Kupeana Zawadi Ukawadia-Mkuu
wa wilaya ya Kahama Mheshimiwa Vita Kawawa akijiandaa kuanza kukabidhi
zawadi kwa washindi katika michezo mbalimbali iliyochezwa uwanjani
Kulia
ni Afisa Miradi Huduma Unganishi kwa jamii kutoka shirika la AGPAHI,
Cecilia Yona akitoa maelezo kuhusu zoezi la utoaji zawadi kwa washindi
katika Bonanza hilo
Mkuu wa wilaya ya Kahama Mheshimiwa Vita Kawawa akimkabidhi zawadi ya begi la shule golikipa bora Damian Adam kutoka Ushetu
Mkuu
wa wilaya ya Kahama Mheshimiwa Vita Kawawa akimkabidhi zawadi ya begi
la shule mfungaji bora wa mpira wa miguu Oscar Onesmo kutoka Kahama Mji
Mshindi
wa shindano la kukimbia na mayai Grace kutoka Kahama Mji akishikana
mkono na mratibu miradi kutoka AGPAHI Dr. Amos Scott
Mchezaji bora Paul George kutoka Ushetu akivaa saa aliyopewa ikiwa ni zawadi ya ushindi
Jesca
Robert kutoka Kahama Mji akishikana mkono na Mkuu wa wilaya ya Kahama
Mheshimiwa Vita Kawawa baada ya kuibuka mshindi katika mchezo wa
kukimbiza kuku upande wa kundi la vijana wa kike
Mkuu
wa wilaya ya Kahama Mheshimiwa Vita Kawawa akimkabidhi zawadi ya saa ya
mkononi neema Bundala kutoka Msalala aliyeshinda katika mbio za mita
100 kwa kundi la vijana wa kike
Vijana wakifuatilia zoezi la utoaji zawadi kwa washindi
Kijana
Patrick Marco kutoka Msalala akiwa ameshikilia zawadi ya soda baada ya
kuibuka mshindi katika shindano la kunywa soda kwa haraka zaidi upande
wa kundi la vijana wa kiume
Kijana
Suzy John kutoka Msalala akiwa ameshikilia zawadi ya soda baada ya
kuibuka mshindi katika shindano la kunywa soda kwa haraka zaidi upande
wa kundi la vijana wa kike
Mkuu
wa wilaya ya Kahama Mheshimiwa Vita Kawawa akikabidhi Kombe kwa Kapteni
wa timu ya mpira wa miguu halmashauri ya Mji Kahama Oscar Onesmo kwa
niaba ya vijana wote wa Kahama Mji.Kombe hilo lilitolewa kwa Halmashauri
iliyoshinda michezo mingi zaidi kuliko halmashauri zingine
Wachezaji wa timu ya vijana kutoka Kahama Mji wakishangilia baada ya kukabidhiwa kombe la ushindi wa jumla
Vijana kutoka Kahama Mji wakiwa na kombe la ushindi wa jumla
Vijana na walezi wa vijana kutoka vituo mbalimbali vya afya wakiwa uwanjani wakishuhudia zoezi la utoaji zawadi
Vijana na walezi wa vijana katika vituo vya afya wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea
Mkuu wa wilaya ya Kahama Mheshimiwa Vita Kawawa akizungumza baada ya kumaliza kutoa zawadi kwa washindi katika bonanza hilo.
Mkuu huyo wa wilaya ya Kahama Mheshimiwa Vita Kawawa pia alitoa zawadi
ya pea moja ya soksi na kalamu kwa kijana aliyehudhuria bonanza hilo la
Michezo
Mkuu
wa wilaya ya Kahama Mheshimiwa Vita Kawawa akifunga bonanza la michezo
ambapo aliwasisitiza vijana kusoma kwa bidii kwani elimu ndiyo ufunguo
wa maisha
Picha ya pamoja-Mgeni
rasmi MheshimiwaVita Kawawa,wafanyakazi wa AGPAHI,halmashauri za
wilaya,walezi wa vijana katika vituo vya afya na vijana kutoka
Halmashauri ya mji wa Kahama
Picha ya pamoja-Mgeni
rasmi Mheshimiwa Vita Kawawa,wafanyakazi wa AGPAHI,halmashauri za
wilaya,walezi wa vijana katika vituo vya afya na vijana kutoka
halmashauri ya wilaya ya Ushetu
Picha ya pamoja-Mgeni
rasmi Mheshimiwa Vita Kawawa,wafanyakazi wa AGPAHI,halmashauri za
wilaya,walezi wa vijana katika vituo vya afya na vijana kutoka
halmashauri ya wilaya ya Msalala
Vijana kutoka halmshauri ya Mji wa Kahama wakiwa katika picha ya pamoja na kombe lao
Vijana
kutoka halmshauri ya Mji wa Kahama wakiwa katika picha ya pamoja na
walezi wao na kombe lao wakiwa wao ndiyo wameshinda michezo mingi
Home
»
»Unlabelled
» AGPAHI Yafanya Bonanza la Michezo la Vijana – Uwanja wa Taifa wa Kahama Mji
Topics:
About Unknown
Kwa jina Naitwa MWEUSI waweza wasiliana nami namba 0757420837, 0629208856 au email: timotheosodoka@gmail.com
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni: