Madaktari
wa Hospitali ya Taifa Muhimbili jana kwa mara ya kwanza wamefanya
upasuaji kwa kutumia darubini (microvascular surgery) wa kuhamisha
misuli na mishipa ya damu kutoka kwenye mguu kwenda sehemu nyingine
chini ya mguu (free gracilis muscle transfer).
Upasuaji
huu wa aina yake na ambao mara nyingi huchukua muda wa saa sita hadi
saba una lengo la kujenga uwezo kwa watalaamu wa ndani ili waendelee
kutoa huduma za ubingwa wa hali ya juu kwa Watanzania wengi zaidi na
vilevile kupunguza kasi ya kupeleka wagonjwa nje.
Mkuu
wa Idara ya Upasuaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) ambaye pia
ameshiriki upasuaji huo Dk Ibrahim Mkoma alisema upasuaji huo unagharimu
kiasi cha dola 40,000 za Marekani nchini Australia ikiwa ni gharama ya
upasuaji tu.
Lengo
kubwa la ushirikiano wa upasuaji huu ni wataalamu kutoka Australia
kuwaachia taaluma ya upasuaji huo madaktari MNH ili iweze kuendelea
kufanya upasuaji huo mbeleni.
Aidha
Dk Mkoma alisema kuwa kuanzia mwakani kutakuwa na utaratibu ambao
utaanzishwa Chuo Kikuu cha Tiba Muhimbili, wa taaluma maalumu ya kusomea
upasuaji wa aina hiyo ili kuweza kupata wataalamu zaidi kutoka nchini.
Alisema hakuna chuo chochote Tanzania kinachotoa taaluma hiyo ya plastic
surgery kwa sasa.
Dk
Mkoma alisema MNH inajivunia kushirikiana na madaktari bingwa kutoka
Australia akiwapo Daktari bingwa James Savundra ambaye ni Rais wa
Madaktari Bingwa wa upasuaji kutoka timu ya upasuaji nchini Australia.
Daktari
bingwa wa upasuaji kutoka Australia, Dk James Savundra alisema upasuaji
huo ni moja ya upasuaji ambao umekuwa ukifanyika kwa gharama kubwa.
Hakuna maoni: