Mufti
Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakari Zuber jana amekabidhiwa ripoti ya
awali iliyoandaliwa na tume ambayo ameiunda kwa ajili ya kufanya
uchunguzi na kuzibainisha mali zote za Baraza kuu la Waislamu
Tanzania (BAKWATA).
Akizungumza
wakati wa kumkabidhi ripoti hiyo, Mwenyekiti wa tume hiyo Sheikh
Abubakari Khalid Hajj alisema kuwa ripoti hiyo imefanyika kwa muda wa
miezi mitatu licha ya kukumbwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ufinyu
wa muda.
Aidha
aliwambia wanahabari kuwa uchunguzi huo umehusisha ufuatiliaji wa mali
za Bakwata katika Mkoa wa Dar es salaam pekee,ikiwemo majengo,viwanja,
pamoja na kupitia mikataba mbalimbali ili kujiridhisha kama imefuata
taratibu za kisheria.
Akizungumza
mbele ya wanahabari mara baadi ya kupokea ripoti hiyo Mufti Mkuu wa
Tanzania Sheikh Abubakari Zuber alisema kuwa ataipitia ripoti hiyo ili
kujua yale yaliyobainishwa na tume yake, na kuahidi kuyafanyia kazi
mapema iwezekanavyo.
Hata
hivyo Mufti huyo ameiongezea muda wa miezi mitatu tume hiyo ambayo ina
jumla ya wajumbe wanane kwa ajili ya kukamilisha kuandaa ripoti ya mkoa
wa Dar es salaam kabla ya kuhamia mikoa mingine kwani zoezi hilo
litafanyika nchi nzima.
Hakuna maoni: