Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda jana aliliagiza jeshi la polisi
kumkamata mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Zavala kata ya Buyuni
Ilala, Chiku Said baada ya kutuhumiwa kuuza viwanja vya watu pamoja na
serikali kinyume na sheria.
Hatua
hiyo imekuja baada ya wananchi kulalamika kwa kumtuhumu mwenyekiti huyo
kuuza viwanja vya serikali kinyume na sheria bila kuwahusisha wajumbe
wenzake hali ambayo imesababisha mgogoro mkubwa wa ardhi katika eneo
hilo
Hatua
hiyo ilimfanya mkuu wa mkoa kumtaka Afisa Ardhi wa Manispaa ya Ilala,
Paul Mbembela kuthibitishwa kuuzwa kwa eneo hilo kinyume na sheria.
“Mkuu
wa mkoa, ni kweli tulikuwa na eneo Block J lakini limeuzwa,” alisema
afisa huyo “Nataka kuwaambia kitu wenyeviti wa mtaa hawaruhusiwi kuuza
eneo katika mtaa. Mimi ningewataka wenyekiti kufuata taratibu za
kisheria zilizowekwa ili kuepuka kutokea kwa hayo mambo,”
Baada
ya kauli hiyo Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Makonda akaliagiza jeshi
la polisi kumkamata mwenyekiti huyo kwa ajili ya uchunguzi zaidi
Hakuna maoni: