Mji huo huenda ulikuwa makao ya wachimbaji na wajenzi wa makaburi
Wanaakiolojia nchini Misri wamegundua kile wanachosema ni mabaki ya mji ambao ulikuwepo zaidi ya miaka 5,000 iliyopita.
Wamepata nyumba, vifaa, vyungu na makaburi makubwa.
Mabaki hayo yamo eneo la ukingo wa mto Nile, karibu na hekalu la Seti, eneo la Abydos.
Wataalamu wanasema makaburi 15 yaliyogunduliwa yanaashiria kwamba ni watu wa hadhi ya juu waliozikwa humo.
Inaaminika kwamba mji huo ulikuwa makao ya maafisa wakuu wa serikali na
wachimbaji na wajenzi wa makaburi, ambao ulifana enzi za kwanza kabisa
za Misri ya kale.
Wataalamu wanasema ugunduzi huo huenda ukasaidia kufufua sekta ya utalii
nchini humo ambayo imeathirika pakubwa kutokana na machafuko
yaliyofuatia kuondolewa madarakani kwa Rais Hosni Mubarak mwaka 2011.Picha inaonesha kile ambacho wataalamu hao wanasema ni makaburi yaliyogunduliwa katika mji huo
Wanaakiolojia wanasema wamegundua vitu vingi kwenye mji huo vikiwemo
majumba, vigae vya vyungu na vifaa vilivyoundwa kwa kutumia chuma na
mawe.
Lakini mtathmini wa BBC wa masuala ya Mashariki ya Kati Alan Johnston anasema muhimu zaidi ni makaburi yaliyogunduliwa.
Inaaminika kwamba maafisa wakuu na wajenzi wa makaburi, ambao huenda
walihusika katika kujenga makaburi ya kifalme katika mji mtakatifu wa
Abydos hapo karibu waliishi eneo hilo. Mji wa ABydos una mahekalu, na
unaaminika kutumiwa kama mji makuu wakati mmoja enzi za kale za utawala
wa Misri.Baadhi ya vitu vilivyogunduliwa eneo ambalo wataalamu wanasema kulikuwa an mji zaidi ya miaka 5,000Maeneo
ya akiolojia karibu na Luxor (pichani) na kwingineko Misri yametatizika
kuwavutia watalii kutokana na misukosuko ya kisiasa
Chanzo-BBC
Hakuna maoni: