Wakazi wa Kata ya Nsemlwa Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi
wanalazimika kulala mapema kutoka na kushikwa na hofu baada ya
nyumba zao wanazoishi kukutwa zimepatwa damu ikiwemo ofisi ya
mtendaji wa kata hiyo damu ambayo haija julikana ni ya
binadamu au ya mnyama nje ya nyumba zao na ndani ya nyumba.
Afisa mtendaji wa kata ya Nsemlwa Jumbe Mselwa aliwaambia
wandishi wa Habari jana kuwa tukio hilo la watu kukuta nyumba
zao zimepakwa damu na watu wasiofahamika limetokea usiku wa
kuamkia Juma pili na usiku wa kuamkia jana hivyo kujenga hofu
kubwa kwa wakazi wa kata hiyo.
Alisema tukio hilo la wakazi wa kata hiyo nyumba zao kupakwa
damu usiku na watu wasiojulikana limetokea kwenye mitaa yake yote
mitano ambapo taarifa hizo zilifikishwa ofisini kwake na
wenyeviti wa wa mitaa hiyo mitano na baada ya kupata taarifa
hizo alilazimika kwenda kuhakikisha na kukuta nyumba hizo zikiwa
zimepakwa damu nje na nyingine ndani ya nyumba .
Jumbe aliitaja mitaa hiyo ambayo nyumba zake zimepakwa damu
kuwa ni Mtaa Kichangani , Migazini ,Kilimani Tulieni na
Mtaa wa Nsenlwa ambao ndio unaongozwa kwa nyumba nyingi
kupakwa damu .
Alisema kutokana na hali hiyo, amewataka wakazi wa kata hiyo
mara wanaopoona kitu ambacho sio cha kawaida watoe taarifa
na mapema kwa uongozi wao wa mitaa wanayoishi .
Mwenyekiti wa Mtaa wa Nsemlwa Adamu Masigati alisema nyumba yake
ni miongoni mwa nyumba ambazo zimepakwa damu na yeye na
wananchi wa Mtaa huo wamekuwa wakijiuliza kwanini tukio hilo
linatokea usiku badala ya mchana .
Akisimulia mkasa huo mmoja wa wananchi waliopatwa na mkasa huo,
Raphael Geoge alisema juzi alikuwa nyumbani kwake majira ya saa
kumi jioni akila chakula ugali sebuleni kwake,lakini aliposhika
tonge la pili ghafla aliona matone mawili ya damu yakidondoka
chini alipokuwa amekaa.
Alisema hali hiyo ilimshitua na kumfanya amwite mtoto wake wa
kike anaitwa Maliselina Joseph ili nae ashuhudie damu hiyo
ambayo haikufahamika imetoka wapi na ni ya mnyama gani.
Majirani wa eneo hilo walifika nyumbani kwa Raphael na kujaa
kwa wingi na walishtushwa na hali hiyo na hasa baada ya kuona
inzi wamejaa kwenye damu hiyo na ndipo walipokwenda kutoa
taarifa kwa uongozi wa serikali ya mtaa.
Mkewe Raphael aitwaye Judith Joseph ambae wakati wa tukio
hilo hakuwepo nyumbani aliporudi nyumbani majira ya saa moja na
nusu usiku alikuta familia yake wakiwa wamekaa kama wagonjwa.
Alisema hali hiyo ilimshtua sana na ndipo alipopewa maelezo
na mme wake juu ya tukio hilo na ndipo alipomshauri mme wake
kuwa wahame kwenye nyumba hiyo hata hivyo mume wake alikataa kwa
kile alichodai kuwa ingekuwa ni nyumba ya kupanga wangehama .
Judith alieleza kuwa kutokana na tukio hilo ana siku mbili
sasa ameshindwa kufanya usafi wa nyumba kutokana na hali ya
hofu na pia tangu siku hiyo wanalazimika yeye na familia
yake kulala mapema muda wa saa mbili usiku .
Nae Wastala Ferusi alisema yeye na familia yake tangu nyumba
yao ilipopakwa damu wamekuwa wakijifungia na kulala mapema na
amekuwa akiwakataza watoto wake kutembea hata kwa majirani.
Alisema tatizo la tukio hilo ni kwamba kama damu haikupakwa nje basi ujue imepakwa ndani ya nyumba.
Hakuna maoni: