DAR ES SALAAM: Video Queen mwenye vituko kila kukicha, Lulu Euggen ‘Amber Lulu’Jumapili iliyopita alibambwa usiku wa manane akifanya vitendo vichafu na msanii wa tamthiya ya Kelele aliyejulikana kwa jina moja la Talik, nje ya ukumbi wa Catalunya uliopo Mwenge Jijini Dar.
Video Queen huyo alikuwa ni mmoja wa waalikwa kwenye sherehe ya kuzaliwa staa wa Bongo Muvi Irene Uwoya, ambapo baada ya kuingia na kupata ulabu kiasi cha kutosha, alitoka nje na kukaa pembeni ya gari akiwa na msanii huyo huku wakipigana mabusu mdomoni bila kujali wapita njia.
“Nyie huyu Lulu atakuwa amepagawa kabisa maana hata haogopi kabisa kama watu wanapita na kuwaona wanachofanya, na wakati huyu sasa hivi anajinadi yuko na Young D” alisikika kijana mmoja akizungumza.
Licha ya binti huyo kuhusishwa na Young D, zipo tetesi pia zinazomtaja msanii wa Hip Hop, Roma Mkatoliki kuwa pia anatoka naye kimahaba.
Hakuna maoni: