Mwanamke
aliyejulikana kwa jina la Stella Apinius (39) mkazi wa mtaa wa Mageuzi
kata ya Ngokolo manispaa ya Shinyanga ameuawa kwa kupigwa na kitu kizito
kichwani na mme wake Ibrahim Daniel (42) kwa kile kilichodaiwa kuwa
amepewa kachumbari iliyochacha.Mwandishi mkuu wa Malunde1 blog,Kadama Malunde,anaripoti.
Tukio
hilo limetokea juzi Januari 17,2017 usiku baada mwanamme huyo
kumshushia kipigo mke wake wa ndoa akidai kuonyeshwa kachumbari ambayo
haikuhifadhiwa vizuri na kupatiwa mboga nyingine aliyodai haina
kiwango.
Inaelezwa
kuwa mwanamme huyo alifika nyumbani akiwa amelewa kisha kuulizia kuhusu
kachumbari ambayo alikula jana yake ndipo mtoto aliyekuwa akimlea
aliyefahamika kwa jina la Elizabeth akamuonesha kachumbari hiyo ambayo
tayari ilikuwa imechacha.
Akisimulia
mkasa huo, mtoto wa marehemu aliyefahamika kwa jina la Daniel Ibrahim
(12) anayesoma darasa la sita katika shule ya msingi Mwadui katika
manispaa ya Shinyanga,alisema baba yake alifika nyumbani saa moja usiku
,alimkuta yeye akiwa na mtoto mwenzie Elizabeth (13) ndipo baba huyo
alipoanza kumhoji Elizabeth kuwa kwanini kachumbari imeharibika.
“Baada ya kuingia ndani baba alimuuliza Eliza kuwa kachumbari aliyoiacha
tarehe 16/1/2017 iko wapi,akaoneshwa baada ya kuiangalia aliiona
imechacha na kuonekana na uchafu, ndipo alitoka nje na kuchukua fimbo
ambayo huwa anaiweka juu ya nyumba na kutaka kuanza kumpiga lakini
kabla ya kumpiga Eliza alichoropoka na kukimbia nje”,alieleza Daniel .
“Baada ya Eliza kukimbia,mama ambaye alikuwa kazini alifika nyumbani,
akamkuta baba akifoka, akauliza kuna nini?,baba akasema kwa nini
hakupika mboga yenye kiwango na kwanini mlipika ugali mwingine wakati
kulikuwa na ugali uliobaki mchana?”,alieleza mtoto huyo.
Aliongeza kuwa kufuatia maswali hayo mama huyo alimjibu mme wake kwa
hasira kuwa kwanini hakuacha pesa nyumbani ili wanunue mboga yenye
kiwango anachotaka yeye majibu ambayo yalimkera baba huyo na kuanza
kumshushia kichapo mke wake.
“Mama alipofika nyumbani baba aliendelea kufoka ndipo mama alimjibu kwa
hasira kwanini hukuacha fedha ya matumizi ya kuweza kupika mboga yenye
kiwango?,ndipo alianza kumpiga kwa kikombe na mateke, akaanguka ndipo
nilikimbia kwa kuwataarifu majirani walikuja na kukuta mama ameanguka
chini ” alifafanua Daniel.
Baadhi ya majirani waliofika katika tukio hilo, Gloria Shija na Leticia
Mashala,walisema walipofika walikuta mlango umefungwa wakaanza kumgongea
ili afungue, alikataa na kusema ana kazi kidogo anaifanya
wasubiri,walichungulia dirishani wakamuona anampuliza puani na masikioni
huku akimmwagia maji ili azinduke,baada ya kuona hazinduki ndipo
alifungua mlango.
Shija alisema waliingia ndani na kumkuta akiwa amemkalisha chini huku
akiwa ameinamisha shingo ambapo walimbeba na kumtoa nje na kujaribu
kummwagia maji tena lakini ilishindikana ndipo walichukua uamuzi wa
kumpeleka hospitalini walifika na kuanza kupimwa lakini alionekana
tayari ameshafariki muda mrefu.
Naye Shangazi wa marehemu Getruda Vitalis alisema wanandoa hao wamekuwa
wakigombana mara mara kwa mara,na wamewahi wamesuluhishwa mpaka kanisani
walikofungia ndoa yao tarehe 14.04.2009.
Kwa upande wake mwenyekiti wa mtaa wa Mageuzi Emmanuel Joshua Sama
chanzo cha mauaji hayo ni kachumbari iliyochacha iliyokuwa imetunzwa
vibaya na mtoto waliokuwa wakimlea Elizabeth na mama alipoingilia
ugomvi huo ndipo akashushiwa kipigo.
“Baada ya baba anayedaiwa kuwa alikuwa amelewa kudai kachumbari
yake,ndipo mama aliingilia kati na mwanamme huyo kumgeuzia kibao,vipimo
vya daktari vinaonesha marehemu alipigwa na kitu kizito kwenye utosi
kichwa kikavimba damu ikavujiandani na alikuwa na michubuko
mikononi”,alieleza Mwenyekiti wa mtaa.
Akizungumza wakati wa misa ya wafu iliyofanyika leo jioni katika kanisa
la Mama Mwenye Huruma lililopo Ngokolo Mjini Shinyanga,Askofu wa kanisa
katoliki jimbo la Shinyanga Mhashamu Liberatus Sangu alieleza
kusikitishwa na mauaji hayo na kutaka kitendo kama hicho kisijirudie
tena katika familia.
"Hili tukio ni baya,linasikitisha,lisijirudie tena katika familia zetu",alisema kwa ufupi.
Msemaji wa familia ya marehemu Baraka Majigwa alisema tukio hilo
limetokana na uzembe wa akina mama kutopaza sauti zao kutokana na
ukatili wanaofanyiwa na waume zao.
"Tukio hili litufumbue macho akina baba na akina mama,akina baba acheni
kuwafanyia ukatili wake zenu,nanyi akina mama acheni kunyamaza
mnapofanyiwa ukatili,naomba pia serikali za mitaa ziwe na kumbukumbu ya
majina ya wanawake wanaofanyiwa ukatili",alieleza Majigwa.
Kaimu kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga Elias Mwita alisema
mtuhumiwa wa mauaji hayo Ibrahim Daniel anashikiliwa na jeshi hilo na
baada ya marehemu kuchunguzwa alionekana kuwa na jeraha katikati ya
kichwa chake.
Mwita alisema uchunguzi wa awali inasemekana chanzo cha mauaji hayo ni
ugomvi wa kifamilia ambao ulikuwa unamhusu Elizabeth ambaye walikuwa
wakimlea kutoka mwaka 2016 na wanaendelea kufanya uchunguzi zaidi kuhusu
kifo hicho.
Mwili wa marehemu umesafirishwa kupelekwa wilayani Ngara mkoani Kagera kwa ajili ya mazishi.
Inaelezwa kuwa ukatili dhidi ya wanawake katika mtaa huo wa Mageuzi umekithiri ambapo hivi karibuni mwanamke mwingine alifariki dunia baada ya kupigwa na mme wake.
Inaelezwa kuwa ukatili dhidi ya wanawake katika mtaa huo wa Mageuzi umekithiri ambapo hivi karibuni mwanamke mwingine alifariki dunia baada ya kupigwa na mme wake.
Mwandishi Mkuu wa Malunde1 blog,Kadama Malunde alikuwepo eneo la tukio ametuletea Picha 40...Tazama hapa chini
Ndani ya kanisa la Mama Mwenye Huruma lililopo Ngokolo Mjini
Shinyanga,Askofu wa kanisa katoliki jimbo la Shinyanga Mhashamu
Liberatus Sangu akiongoza misa ya wafu kwa ajili ya kumwombea marehemu
Stella Apinius
Picha ya marehemu Stella Apinius ikiwa kwenye jeneza
Misa inaendelea
Misa inaendelea
Misa inaendelea
Waumini wakiwa kanisani
Askofu Sangu akimwombea marehemu Stella Apinius
Askofu Sangu akimwombea marehemu
Waumini,ndugu wa marehemu na watu mbalimbali wenye mapenzi mema wakiwa kanisani
Wanakwaya wakiwa kanisani
Masisita wakiaga mwili wa marehemu
Ndugu,jamaa na marafiki wakiaga mwili wa marehemu
Misa inaendelea
Zoezi la kuaga mwili wa marehemu kanisani likiendelea
Wanakwaya wakiaga mwili wa marehemu
Mtoto Elizabeth aliyekuwa analelewa katika familia ya marehemu.
Ndugu wa marehemu wakiaga mwili wa mpendwa wao
Askofu Liberatus Sangu akizungumza wakati wa misa ya kuombea wafu
Askofu Sangu aliiasa jamii kuachana vitendo viovu na kutaka tukio kama hilo la mauaji lisijirudie tena katika familia
Askofu Sangu akimwombea marehemu
Askofu Sangu akiomba kanisani
Mwili wa marehemu ukitolewa kanisani
Mwili ukiwa nje ya kanisa
Mwili wa marehemu ukiwa kwenye gari kwa ajili ya kupelekwa nyumbani
kwake mtaa wa Mageuzi kata ya Ngokolo katika manispaa ya Shinyanga
Mamia ya wakazi wa Shinyanga wakiwa nje ya kanisa
Mwili wa marehemu ukiingizwa ndani ya nyumba ya marehemu katika mtaa wa Mageuzi kata ya Ngokolo
Waombolezaji wakiwa nyumbani kwa marehemu
Wakazi wa Mtaa wa Mageuzi wakiwa nyumbani kwa marehemu
Wakazi wa mtaa wa Mageuzi wakiaga mwili wa marehemu
Zoezi la kuaga mwili wa marehemu likiendelea nyumbani
Mtoto wa marehemu Daniel Ibrahim(mwenye nguo nyeusi) akiwa na ndugu zake msibai
Kulia ni Balozi wa Ubalozi wa Mageuzi Juu,Samwel Shija Ng'hwaya akizungumza msibani
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Thoma Mtume John Kapelembe akitoa salamu za rambirambi
Mwenyekiti wa mtaa wa Mageuzi Emmanuel Joshua akizungumza msibani
Mwenyekiti wa mtaa Emmanuel Joshua akizungumza
Msemaji wa familia Baraka Majigwa akizungumza
Kulia ni rafiki yake na marehemu Maria Lusambo ambaye ameachiwa jukumu
la kuangalia nyumba ya marehemu akiteta jambo na shangazi yake na
marehemu Getruda Vitalis
Mwenyekiti wa mtaa wa Dome katika kata ya Ndembezi Solomoni Naringa
Najulwa akielezea namna mtoto Eliza(aliyemshika) alivyoanza kulelewa na
marehemu baada ya kukosekana wazazi wake na sasa mlezi wake amefariki
Mwenyekiti
wa mtaa wa Dome katika kata ya Ndembezi Solomoni Naringa Najulwa
aliwashukuru ndugu wa marehemu kukubali kumlea mtoto Eliza na kama
watashindwa basi waitarifu serikali ili iweze kumlea mtoto huyo.
Hakuna maoni: