MKAZI
wa Kijiji cha Kimelembe wilayani Ludewa, mkoani Njombe, Maria Kayombo
(31) amenusurika kifo baada ya kunywa maji ya betri kutokana na wivu wa
kimapenzi.
Akizungumza jana, mama mzazi wa mwanamke huyo Magdalena Kayombo alisema
tukio hilo lilitokea juzi ambapo alipigiwa simu akiwa shambani kuwa hali
ya mtoto wake ni mbaya baada ya kunywa sumu.
Alisema walimkimbiza katika zahanati ya jirani ambapo alipatiwa matibabu
na kumweleza kuwa alikuwa amekunywa maji ya betri baada ya kugombana na
mumewe, Peter Henjewele akimtuhumua kuwa na ‘mchepuko’.
“Sikuweza kumhoji sana kwani nilishikwa na mshangao aliponiambia
amekunywa maji ya betri ili afe amuache mumewe aendelee kuwa na
mchepuko,” alisema.
Akizungumzia hali hiyo baada ya kupata nafuu mwanamke huyo alisema
chanzo cha yeye kuchukua uamuzi huo ni kitendo cha mume wake kuwa na
wanawake wengine nje.
“Tulianza nae maisha katika hali ngumu, kitendo cha kuanza kuchepuka
wazi wazi na wanawake wengine ni dharau nikaona bora nife kuliko
kuvumilia maumivu hayo ya kimapenzi,” alisema.
Hata hivyo, mume wa mwanamke huyo, alitokomea kusikojulikana baada ya kuona mke wake amekunywa maji ya betri.
Chanzo-Mtanzania
Hakuna maoni: