Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli
anatarajia kuwasili mkoani Shinyanga Januari 12,2017 kwa ajili ya
kuadhimisha siku ya Mapinduzi ya Zanzibar pamoja na kuwasalimia wananchi
wa mkoa wa Shinyanga.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack
amesema rais Magufuli atazungumza na wakazi wa Shinyanga siku ya
Alhamis mchana Januari 12,2017 katika uwanja wa CCM Kambarage mjini
Shinyanga.
Mkuu huyo wa mkoa amewaomba wakazi wa Shinyanga kujitokeza kwa wingi kumpokea mheshimiwa rais.
Maadhimisho ya siku ya Mapinduzi ya Zanzibar kitaifa yatafanyika Zanzibar.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake leo Jumatatu Januari 9,2017
Waandishi wa habari wakiwa katika ofisi ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga leo mchana Januari 9,2017
Waandishi wa habari wakiwa ofisini kwa mkuu wa mkoa wa Shinyanga
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack akizungumza na waandishi wa habari
Hakuna maoni: