Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Muliro Jumanne Muliro.
***
Jeshi
la polisi mkoa wa Shinyanga linamshikilia mwanamme mmoja (55) jina
linahifadhiwa kwa tuhuma ya kumbaka mtoto wake mwenye umri wa miaka 09
,mwanafunzi wa darasa la awali katika shule ya msingi Ngundangali
wilayani Kishapu mkoani humo.
Akielezea
kuhusu tukio hilo kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga,ACP Muliro
Jumanne Muliro alisema Mei 18,2017 saa nne asubuhi mwalimu mkuu wa shule
hiyo alibaini kuhusu ukatili aliofanyiwa mwanafunzi huyo na baba yake
mzazi mkazi wa kijiji cha Uchunga kata ya Uchunga wilayani humo.
“Mwalimu
mkuu alibaini kuwa mtoto huyo amebakwa baada ya mwanafunzi huyo
kulalamika kuwa amebakwa na baba yake mzazi”,alieleza kamanda Muliro.
Kamanda
Muliro alisema chanzo cha tukio hilo ni imani za kishirikina na kwamba
tayari mtuhumiwa anashikiliwa na jeshi la polisi na mtoto amelazwa
katika hospitali ya wilaya ya Kishapu na hali yake inaendelea vizuri.
Hata
hivyo alisema jeshi hilo pia linamsaka mganga wa kienyeji aliyemshauri
mtuhumiwa kubaka mtoto wake ili apate utajiri ili kila mmoja ashtakiwe
kwa nafasi yake ya kihalifu.
Hakuna maoni: