WIKI chache baada ya shabiki wa msanii wa muziki nchini Nigeria, David
Adeleke (Davido), Chiamaka Okeke kutangaza kujiua ifikapo Agosti 13
ambayo ni siku yake ya kuzaliwa endapo hatakutana na Davido, ni bahati
kwamba Davido amekubali kukutana na shabiki huyo siku yake ya kuzaliwa.
Davido amesema yupo tayari kuhudhuria siku hiyo ya kuzaliwa kwa shabiki
yake huyo ili kuweza kuokoa maisha yake baada ya kuona malalamiko ya
shabiki wake huyo aliyesema tangu 2014, alijaribu kutuma ujumbe, lakini
hakufanikiwa kujibiwa wala kukutana naye.
Hakuna maoni: