Michael Silanda ( 26 ) mkazi wa kijiji cha Ibindi, tarafa
ya Nsimbo wilaya ya Mlele mkoani Katavi amefariki dunia baada
ya kunywa pombe ( Viroba ) aina ya Zed kupita kiasi bila kula
chakula….
Kamanda wa polisi mkoani Katavi,Kamishna Msaidizi
Mwandamizi,Dhahiri Kidavashari amesema tukio hilo limetokea wiki
iliyopita majira ya saa sita usiku kijijini hapo…..
Alisema siku ya tukio marehemu baada ya kuamka asubuhi
nyumbani kwake hapo majira ya saa tano asubuhi alielekea kwenye
baa ambayo ilikuwa ikiuza vinywaji vya aina mbalimbali
zikiwemo pombe kali….
Alifafanua kuwa,baada ya kufika kwenye baa hiyo aliwakuta
baadhi ya wanakijiji wenzake wakiwa wanakunywa pombe za aina
mbalimbali hali ambayo ilimfanya marehemu aweze kujumuika nao
kwa kuagiza pombe aina ya Zed…
Alisema Michael aliendelea kunywa viroba kuanzia muda huo
kwenye baa hiyo bila kula kitu chochote hadi majira ya saa
sita usiku alipoamua kurudi nyumbani kwake huku akiwa amelewa
pombe kupita kiasi….
Baada ya kufika nyumbani kwake aliingia ndani ya nyumba
yake na kulala bila kula chakula cha aina yoyote na siku
iliyofuata majira ya saa mbili asubuhi ndipo walipomkuta
Michael akiwa amefariki huku akiwa amelala kitandani kwake,…..
Kamanda Kidavashari alisema uchunguzi wa awali uliofanywa
kuhusiana na tukio hilo umebaini kuwa kifo hicho kimesababishwa
na marehemu kunywa pombe nyingi kupita kiasi bila kula
chakula….
Hakuna maoni: