Wakati taharuki iliyosababishwa na mlipuko wa homa ya dengue
ikiendelea kutikisa kila kona ya jiji, imebainika kwamba gharama za
vipimo katika hospitali mbalimbali zinafikia Sh50,000, ikiwa ni tofauti
kubwa na Sh1,000 kwa kipimo cha malaria.
Ugonjwa huo unazidi kusambaa jijini Dar es salaam na baadhi ya
mikoa, kiasi cha mamlaka kuagiza mabasi yote yaendayo mikoani yafanyiwe
usafi wa kunyunyizia dawa za kuua wadudu kudhibiti usienee zaidi
mikoani. Pia wananchi wameshauriwa kuvaa nguo ndefu ili kudhibiti mbu
wanaoeneza ugonjwa huo mchana tofauti na mbu wa malaria.
Hakuna maoni: