Mnamo tarehe 11/06/14 majira ya 0100hrs huko kituo kidogo cha
Kimanzichana Pwani,watu wasiojulikana waliojifanya kuwa ni raia wema
waliingia kituo kidogo cha Polisi Kimanzi Chana huku wakikimbia wakiwa
na silaha za jadi kiasi cha askari wa zamu kuamini kuwa ni watu
wanaohitaji msaada.
Cha kushangaza watu hao walimvamia askari mwenye silaha ambaye
amefahamika kwa jina la JOSEPH NGONYANI na kuanza kumkatakata mapanga na
hatimaye kupora silaha aina ya SMG ikiwa na risasi 30.Ndipo walipoanza kushambulia kwa risasi askari wengine na kufanikiwa kupora SMG ya pili na risasi 30. Hatimaye watu hao wakapora risasi za akiba 41 na kutoweka kusikojulikana.
Askari Ngonyani alifariki dunia alipokuwa anapatiwa matibabu kwenye
hospitali ya wilaya ya Mkuranga. Askari mwingine aitwaye VENANCE
amejeruhiwa mgongoni kwa risasi ambayo bado imo ndani, na kwenye paja la
mguu wa kulia.
Mgambo Mariam alijeruhiwa kichwani, shingoni na kuvimba bega kutokana na kupigwa sana mateke na kujeruhiwa mbavuni.
Kwa mujibu wa mganga Mkuu wa zamu wa Hospitali hiyo aitwaye
VERONICA MUSIME, anathibitisha askari huyo kufariki akiwa anapatiwa
matibabu hapo Mkuranga wakati wengine wamekimbizwa Muhimbili kwa
matibabu ya kina.
Kazi ya Mungu haina makosa; vituoni tuwe makini sana na staili hii
ya ujambazi; HESHIMA PEKEE kwa marehemu na majeruhi hawa ni
kuwapata watuhumiwa wote na silaha walizoiba bila kuchelewa. Bila kujali
mkoa ulipo, taarifa za haraka tunatarajia kupata toka kwako kuhusiana
na wahusika wa tukio hili. AMEN
Hakuna maoni: