Waziri
wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi Profesa Anna Tibaijuka
amenusurika kifo baada ya gari alilokuwa akisafiria kutoka Wilayani Muleba kwenda
Dodoma kugonga punda katika kijiji cha Wendele Wilayani Kahama
Mkoani Shinyanga
Mashuhuda wa tukio hilo walisema lilitokea jana majira ya saa 11 jioni ambapo gari lenye
namba za usajili STK 5857mali ya Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya
makazi lililokuwa likiendeshwa na dereva Linusi Eliasi (42) liligonga punda aliyekatiza ghafla barabarani.
Akielezea
zaidi kuhusu ajali hiyo kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga
Kihenya Kihenya amesema Waziri Tibaijuka alikuwa na baadhi ya
wanafamilia wake katika gari hilo wakitoka Muleba kwenda Dodoma kwa
ajili ya kuwahi shughuli za Bunge zinazoendelea ,Hata hivyo hakuna alie jeruhiwa nampaka sasa waziri yupo vizuri.
GARI YA WAZIRI TIBAIJUKA
Hakuna maoni: