Katika
hali ya kushangaza na kusikitisha sana, kikongwe mmoja aitwaye Athuman
Ngusa Kulaba (80) amekuwa akiishi kwa kula udongo wa nyumba anayoishi
kwa sababu ya kukosa chakula cha kibinadamu.
Kikongwe
huyo alikutwa na Uwazi hivi karibuni nyumbani kwake, Chanika wilayani
Ilala, Mkoa wa Dar es Salaam baada ya majirani kusema kwamba wamekuwa
wakimshuhudia akipata mlo huo kwa karibu mwaka mmoja sasa.
Baada
ya kuona hali yake inazidi kuwa mbaya, mjumbe wa eneo hilo, John
Kanguya na majirani zake walimchukuwa hadi kwenye Kituo cha Afya cha
Chanika kwa ajili ya kumpima afya yake ambapo madaktari walisema tayari
alipatwa na ugonjwa wa safura ambapo tumbo lake limejaa minyoo.
Uwazi lilishuhudia sehemu kubwa ya ukuta wa nyumba anayoishi kikongwe huyo ikiwa imemeguka kwa ajili ya kuchimbuliwa na kuliwa.
Majirani
walilieleza Uwazi kwamba, nyumba anayoishi kikongwe huyo aliachiwa
kuilinda na mtu aliyetajwa kwa jina moja la Musada karibu miaka 20
iliyopita bila kupewa huduma nyingine zikiwemo fedha.
Akizungumza na Uwazi kwa lugha ya Kisukuma, kikongwe huyo alikiri kuwepo kwenye nyumba hiyo kwa miaka 20.
Alisema awali alikuwa akipewa pesa na tajiri yake lakini baadaye utaratibu huo ukafa hivyo kwa sababu ya kukosa pesa ya kujikumu ndiyo akaamua kula vyakula vya ajabu, ukiwemo udongo wa ukuta wa nyumba hiyo.
Alisema awali alikuwa akipewa pesa na tajiri yake lakini baadaye utaratibu huo ukafa hivyo kwa sababu ya kukosa pesa ya kujikumu ndiyo akaamua kula vyakula vya ajabu, ukiwemo udongo wa ukuta wa nyumba hiyo.
Alisema
anawashukuru majirani wa eneo hilo ambao wameweza kutambua maisha
magumu anayoishi na kuamua kumpeleka hospitali na kumsaidia chakula.“Kwa sasa naomba Watanzania wenzangu wanisaidie nauli ili niweze kurudi kwetu Bukene, Tabora, maisha hapa ni magumu sana,” alisema kikongwe huyo.
Hakuna maoni: