Familia ya Marehemu Joseph Mungai ikiwa imeshikana mkono ishara ya
upendo wakati wa mazishi ya baba yao mjini Mafinga wilaya ya Mufindi
mkoa wa Iringa.
Baadhi ya waombolezaji wakiwa katika mazishi ya Mzee Joseph Mungai huko Mafinga wilaya ya Mufindi mkoa wa Iringa.
Waziri mkuu mstaafu Mhe. Frederick Sumaye akitoa salama zake kwa
niaba ya mwenyekiti wa Taifa wa Chadema katika mazishi ya Mzee Joseph
Mungai huko Mafinga wilaya ya Mufindi mkoa wa Iringa.
Mbunge wa Singida Mashariki Mhe. Tundu Lissu na waombolezaji wengine
wakitoa heshima za mwisho katika mazishi ya Mzee Joseph Mungai huko
Mafinga wilaya ya Mufindi mkoa wa Iringa.
Mbunge wa Mikumi Mhe. Joseph Haule akitoa heshima zake za mwisho
Waziri wa Ardhi Nyumba na maendeleo ya makazi Mhe. Wiliam Lukuvi
akiteta jambo na mbunge wa Singida Mashariki Mhe. Tundu Lissu wakati wa
mazishi ya marehemu Mungai.
*****
WAZIRI wa Ardhi Nyumba na maendeleo ya makazi ,Wiliam Lukuvi aongoza
mamia ya waombolezaji katika mazishi ya aliyekuwa waziri wa Elimu na
mbunge wa mstaafu wa jimbo la Mufindi kaskazin Joseph Mungai.
Akizungumza katika ibada ya mazishi leo mjini Mafinga wilaya ya
Mufindi Lukuvi ambae alimwakilisha Rais Dkt John Magufuli alisema
kuwa Mungai atakumbukwa kwa uongozi wake uliotukuka hasa katika
misingi mizuri ya elimu wa Elimu ya Sekondari (MMES).
Lukuvi alisema kuwa wakati serikali ilipoanzisha suala la Sekondari za
Kata, Mafinga na Mufindi kwa ujumla mwamko huo ulishaanza toka miaka ya
1980 ambayo kwa uongozi wake kama Mbunge alihamasisha Wananchi kutoa
michango, kufyatua matofalina kina mama kuchota maji yote hiyo nji
katika kufanikisha adhima ya kusogeza elimu ya sekondari kwa watu
wengi.
“Alianza kuwa kiongozi akiwa na umri mdogo kuliko wanasiasa wote wa Mkoa
wa Iringa wakati huo, lakini pia alikuwa kiunganishi pale kunapotokea
misuguano yoyote hakuwa na makuu na kama ulikuwa ukitaka ushauri basi
utaupata kwa mzee wetu mungai ,” alisema.
Akiongoza ibada ya mazishi askofu wa KKKT dayosisi ya Iringa Dkt
Owdenburg Mdegella alisema kuwa kila mwanadamu aishie chini ya hili jua
anapaswa kuishi maisha ya kumuabudu mungu na kuachana na tabia ya
kuhukumiana hapa duniani kwakuwa kila mtu atajibu dhambi zake akiwa
mbinguni.
Dkt Mdegela alisema Mungai ni moja kati ya viongozi wachache waioacha
historia kubwa hapa nchini kutokana na uongozi wake uliotukuka wa
kupigania maendeleo ya watanzania bila ya ubaguzi wa aina yoyote.
“Leo tumempoteza mtu muhimu sana ndugu yangu Lukuvi...mimi na wewe
tunapaswa kukaa chini na kuangalia mustakabali wa mkoa wetu wa Iringa.
Ameondoka mzee Peter Siyovvela ameondoka Adam Sapi na leo ameondoka
mzee wetu Mungai sasa ni wakati wetu kwani kwa Iringa tumebaki mimi na
wewe sasa tukutane kabla mwaka haujaisha ili kujadili jambo hili
alisema” Mdegella
SUMAYE
Akizungumza kwa niaba ya Mwenyekiti wa chama cha Demokrasia na
maendeleo Chadema Waziri Mkuu mstaafu Mhe. Fredrick Sumaye alisema kuwa
Taifa la Tanzania kimepoteza kiongozi makini aliyekuwa na uthubutu wa
kutenda mambo bila ya ubaguzi na kusimamia kile anacho kiamini katika
kuwatumikia watanzania.
Alisema kuwa Mungai alikuwa ni mtu mchapakazi aliyekuwa na hoja
alizozijenga na kuzisimamia kikamilifu kwani alitamani sana kutenda
mambo kwa haki bila ya kubaguana kiitikadi bali alisimama katika haki.
Alisema kuwa chama cha demokrasia na maendeleo chadema kimesikitiswa
sana na kifo chake kwani alikuwa ni mtu mpenda demokrasia hivyo katika
muuenzi na kutambua mchango wake Hapa nchini watanendeleza kudumisha
misingi mizuri ya demokrasia aliyokuwa akiishi marehemu Mungai
Luhavi
Kwa upande wake Naibu Katibu mkuu wa chama cha mapinduzi Rajabu Luhavi
alisema Mungai atakumbukwa kwa uongozi wake uliotukuka kwa wa
kuwatumikia watanzania bila ya ubaguzi.
“Alikuwa kiongozi mzuri tangu uongozi wa Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu
Julius Nyerere. Ametoa mchango mkubwa kwenye maendeleo ya nchi yetu.
Tunapaswa kuenzi yale mazuri waliyoyafanya na sisi tunaanzia pale
alipoishia.
Akizungumza wasifu wa marehemu Denis Mungai alisema kuwa Mungai aliwahi kuwa Mbunge wa Mufindi kupitia CCM kwa miaka 35.
Pia amewahi kushika nyadhifa mbalimbali serikalini enzi za utawala wa
Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere na pia katika awamu za
pili, tatu na nne.
Baadhi ya nyadhifa alizowahi kushika kwa nyakati tofauti ni uwaziri wa
iliyokuwa Wizara ya Elimu na Utamaduni, Waziri wa Kilimo na Maendeleo ya
Mifugo na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi.
Wabunge
Baadhi ya wabunge wa majimbo ya Mkoa wa Iringa wakizungumzia Mungai huku
kila mmoja akisema alikuwa kiongozi mkweli aliyesimamia alilokuwa
analiamini.
Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa (Chadema), alisema Mungai alikuwa kiongozi wa wazi asiyegopa kusimamia ukweli.
Alisema amepokea kwa mshtuko taarifa ya msiba huo na kubainisha kuwa alimfahamu Mungai akiwa nje ya ulingo wa siasa.
“Alikuwa kiongozi mzuri tangu uongozi wa Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu
Julius Nyerere. Ametoa mchango mkubwa kwenye maendeleo ya nchi yetu,
tunapaswa kuenzi yale mazuri waliyoyafanya na sisi tunaanzia pale
alipoishia.
“Alikuwa kiongozi muwazi na alituunga mkono wapinzani ingawa hakushinda…
kwa ujumla alikuwa mtu mkweli asiyefungamana na siasa za upande
wowote,” alisema Msigwa.
Mbunge wa Mafinga mjini Cosato Chumi alisema kuwa watu wa Mafinga na
Mufindi kwa ujumla wamempoteza mtu muhimu sana kwani atakumbukwa kwa
mengi aliyofanya hasa mwamko na kuisogeza elimu ya sekondari kwa watu
wa kawaida kupitia Mufindi Education Trust-MET.
Chumi alisema kuwa wakati serikali ilipoanzisha suala la Sekondari za
Kata, Mafinga na Mufindi kwa ujumla mwamko huo ulishaanza toka miaka ya
1980 ambayo kwa uongozi wake kama Mbunge alihamasisha Wananchi kutoa
michango, kufyatua matofali na kina mama kuchota maji katika
kufanikisha azma ya kusogeza elimu ya sekondari kwa watu wengi.
“Kwa jitihada zake mzee Mungai Mufindi ndio Wilaya ya Kwanza hapa
nchini kuwa na Bank ya Wananchi yaani Community Bank (Mucoba) ambayo
imeendelea kuwa kimbilio la tabaka la chini na Kati katika suala zima la
mikopo na huduma za kibenki.
"Mimi nawaombea faraja wanafamilia wote katika kipindi hiki cha majonzi.
Mungu ailaze Roho yake Mahali Pema Peponi - Amina alisema Chumi ”.
Picha na Habari kwa hisani ya MatukiodaimaBlog
Hakuna maoni: